Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Makala»Ratiba Ya Usaili Ajira Mpya za Walimu 2024/2025
Makala

Ratiba Ya Usaili Ajira Mpya za Walimu 2024/2025

Kisiwa24By Kisiwa24January 2, 2025No Comments3 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Hii Hapa Ratiba Ya Usaili Ajira Mpya za Walimu 2024/2025, Habari, Je wewe ni mwombaji wa ajira mpya za ualimu kupitia tovuti ya Ajira portal basi unahitaji kufahamu Ratiba ya usaili iliyotolewa na Sekretalieti ya Ajira katika utumishi wa UMMA.

Taarifa Kuhusu Usaili Wa Kada Za Ualimu

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 iliyorejewa 2019, ambayo inaelekeza kuwepo kwa chombo maalumu cha kushughulikia mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma.

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilitoa taarifa ya kusitishwa usaili wa Walimu tarehe 17 Oktoba, 2024 ambapo taarifa hiyo ilitokana na tangazo la kuitwa kwenye usaili la terehe 15 Oktoba, 2024. Hivyo, kupitia tangazo hili, Katibu wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwatangazia waombaji kazi wote wa Kada za Ualimu ambao usaili wao ulisitishwa kwa muda kuwa usaili huo utafanyika kuanzia
terehe 14 Januari, 2025 mpaka tarehe 24 Februari, 2025. Ratiba ya usaili huu itapatikana katika Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira (www.ajira.go.tz) na mitandao rasmi ya kijamii ya Taasisi. Vile vile, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawajulisha wasailiwa wote wa kada za ualimu kuwa, usaili wa kuandika (mchujo) na mahojiano ya ana kwa ana utafanyika ndani ya mikoa wanayoishi wasailiwa na watapangiwa vituo vya kazi kulingana na ufaulu wao popote nchini.

Hivyo basi, waombaji kazi wa kada za ualimu na wale walioomba kwa ajili ya kada za amali na biashara mnatakiwa kuhuisha taarifa za makazi ya sasa (current physical address) kwenye mfumo wa ‘Ajira Portal’ ili muweze kupangiwa kituo cha kufanyia usaili jirani na maeneo mnayoishi kwa sasa. Tangazo la majina kuonesha mtakapofanyia usaili
litatolewa tarehe 06 Januari, 2025 kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, mitandao rasmi ya kijamii ya Taasisi na akaunti za waombaji kazi kwenye mfumo wa ‘Ajira Portal’. Vilevile wale wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa waje na vyeti vyao halisi vya taaluma, Cheti cha Kuzaliwa pamoja na kitambulisho halisi kwa ajili ya Utambuzi.
Vitambulisho vinavyotambulika ni pamoja na; kitambulisho cha Uraia (NIDA), kitambulisho cha Mkazi, kitambulisho cha Mpiga kura, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Kazi, Barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa unaoishi au Sheha. Aidha, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawakumbusha watafuta fursa za ajira wote kuwa mchakato wa ajira unaendeshwa kwa kuzingatia
misingi ya Sifa, Haki, Usawa na Uwazi hivyo mnapaswa kujiepusha kutoa rushwa na kupokea taarifa potofu.

Ratiba Ya Usaili Ajira Mpya za Walimu 2024/2025

Hapa chini ni ratiba kamili ya usaili wa Ajira za Ualimu kwa mwaka wa 2024/2025.

Bonyeza HAPA kudownload Ratiba Yote

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleVIINGILIO Mechi ya Yanga vs TP Mazembe 04 January 2025
Next Article Kikosi cha simba kilicho safiri kuelekea TUNISIA
Kisiwa24

Related Posts

Makala

Jinsi ya kupika Pilau kwenye Rice Cooker

October 9, 2025
Makala

Jinsi ya Kuwasha Rice Cooker

October 9, 2025
Makala

Jinsi ya kupika Maharage kwenye Rice cooker

October 8, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
  • NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited
  • NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania
  • NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • NAFASI za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025783 Views

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

July 12, 2025531 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025445 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.