WALIO CHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2025

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Ratiba na Nauli ya MV Victoria Hapa Kazi Tu Kutoka Mwanza Kwenda Bukoba

Filed in Makala by on November 4, 2024 0 Comments

MV Victoria Hapa Kazi tu Nauli na Ratiba Kutoka Mwanza Hadi Bukoba

Fahamu Kuhusu Ziwa Vitoria

Ziwa Victoria, Ni moja miongoni mwa maziwa makubwa zaidi Tanznia na Afrika, limekuwa kitovu cha usafiri wa majini kwa miongo mingi kati ya mkoa wa Mwanza na wilaya ya Bukoba. Leo katika makala hii tutaenda kukupa ufahamu zaidi juu ya nauli na ratiba ya meli mpya ya MV Victoria Hapa Kazi tu inayofanya safari zake kati ya mwanza na Bukoba.

MV Victoria Hapa Kazi tu hii ni meli ya kisasa iliyozinduliwa hivi karibuni, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo. Imejengwa kwa viwango vya juu vya kimataifa, ikiwa na vyumba vya daraja la kwanza, la pili na la tatu. Meli hii inaonyesha hatua kubwa ya maendeleo katika sekta ya usafiri wa majini Tanzania.

Ratiba na Nauli ya MV Victoria Hapa Kazi Tu

Ratiba ya Meli ya Mv Victoria Hapa Kazi Tu Kati ya Mwanza na Bukoba

Hapa tunaenda kutazama ratiba ya meli ya Mv Victoria hapa kazi tu inayofanya safarri zake katika ziwa victiria kati ya Mwanza na Bukoba

1. Kutoka Mwanza Kwenda Bukoba Kupiti Bandari ya Kemondo

  • Meli huanza safari yake kunako majira ya saa 3:00 usiku kwa siku za Jumanne, Alhamisi na Jumapili

2. Kutoka Bukoba Kwenda Mwanza Kupitia Bandari ya Kemondo

  • Meli huanza safari zake kuanzia majira ya 3:00 Usiku kila siku kwa siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa

Kumbuka wasafili wanakumbushwa kufika bandarini iwe kwa upande wa Mwanza au Bukoba mapema iwezekanavyo lisaa limoja kabla ya meli kuanza safari ili kuepusha usumbufu usio wa lazima. Mchakato wa kupanda katika meli ni wa kuridhisha na wenye utaratibu mzuri sana kwani maafisa wa usalama katika bandari husimamia zoezi la kuhakikisha kila abiria ana tiketi halali na mizigo yao inakaguliwa ipasavyo.

Ratiba na Nauli ya MV Victoria Hapa Kazi Tu

Ratiba na Nauli ya MV Victoria Hapa Kazi Tu

Nauli Harisi Za Meli Ya Mv Victoria Hapa Kazi Tu

Kama unatarajia kusafiri kati ya Mwanza na bukoba kwa kutumia usafiri wa maji kwa meli ya Mv Victoria hapa kazi tu basi ni muhimu pia kufahamu nauli za usafri huo kutoka Mwanza hadi Bukoba na kutokea Bukoba hadi Mwanza.

Nauli za meli ya Mv Victoria Hapa Kazi zimepangwa kwa kuzingatia vitu vifuatavyo

  1. Daraja la meli
  2. Umri wa Abiria

Sasa tutazame mgawanyo wa nauli katika meli ya Mv Victoria hapa kazi tu inayofanya safari zake katika ziwa Victoria kwa kuunganisha maeneo ya Mwanza na Bukoba.

1. Nauli ya Daraja la Uchumi

  • Nauli ya watu kuanzia miaka 18 na kuendelea ni Tsh 21,000
  • Nauli ya wat0t0 wenye umri wa miaka chini ya 18 ni Tsh. 11,000

2. Nauli ya Daraja la Biashara

  • Nauli ya watu kuanzia miaka 18 na kuendelea ni Tsh. 40,000.
  • Nauli ya wat0t0 wenye umri wa miaka chini ya 18 ni Tsh. 20,500.

3. Nauli ya Daraja la Kwanza

  • Nauli ya watu kuanzia miaka 18 na kuendelea ni Tsh 55,000.
  • Nauli ya wat0t0 wenye umri wa miaka chini ya 18 ni Tsh.28,000.

Huduma Zitolewazo Ndani ya Meli Ya Mv Victolia Hapa Kazi Tu

  • Vyakula
  • Vinywaji
  • Vyumba vya kulala
  • Kutizama luninga (Tv)
  • Vitafunwa
  • Upatikanaji wa Mawasiliano mda wote wa Safari

Hali ya Usalama Katika Meli Ya Mv Victolia hapa Kazi Tu

Usalama ndani ya meli umepewa kipaumbele cha juu hii ni kutokana na ajairi ya meli ya Mv Victoria kitu kilicho chochea maboresho ya hali ya juu ya kiusalama katika meli hii ya kisasa zaidi

  • Kuna vifaa vya kutosha vya kuokolea maisha, pamoja na boti za kuokolea.
  • Mabaharia wenye uzoefu na mafunzo ya kutosha.
  • Meli imefungwa mfumo wa GPS na rada za kisasa.

Hitimisho

MV Victoria Hapa Kazi tu si tu njia ya usafiri, bali ni ishara ya maendeleo ya Tanzania katika sekta ya usafiri wa majini. Imeboresha kwa kiasi kikubwa uhusiano wa kibiashara na kijamii kati ya mikoa ya Mwanza na Kagera, huku ikitoa huduma bora na ya kuaminika kwa wasafiri. Safari hii inathibitisha kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa katika kuboresha miundombinu ya usafiri, huku ikidumisha viwango vya juu vya usalama na starehe kwa wasafiri wake. MV Victoria Hapa Kazi tu ni mfano mzuri wa jinsi uwekezaji katika sekta ya usafiri wa majini unavyoweza kuleta tija kwa jamii nzima.

Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa unamaswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.

Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku

BONYEZA HAPA

MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *