Ratiba Mpya ya Ligi Kuu NBC 2024-2025 Raundi ya Pili, Ratiba Ligi kuu ya NBC Bara Mzunguko wa Pili 2024/2025, Ratiba ya NBC Premier League Roundi ya 2 2025, Hii hapa ratiba mpya ya NBC 2024/2025 kwa mzunguko wa roundi ya Pili. BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza mabadiliko ya tarehe ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo hapo awali ilipangwa kuendelea Machi 1, 2025 baada ya kutamatika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi na fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Ratiba Ligi kuu ya NBC Bara Mzunguko wa Pili 2024/2025
Michezo ya Ligi Kuu ya NBC itarejea katika juma la kwanza la Februari, 2025 kwa michezo ya ‘viporo’ kabla ya kuendelea na michezo ya mzunguko wa 17. Tarehe rasmi pamoja na ratiba iliyofanyiwa maboresho, zitatangazwa hivi karibuni.
Mabadiliko ya Ratiba kwa Mujibu wa CAF
Mabadiliko hayo yamekuja baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kusogeza mbele fainali za CHAN kutoka Februari 1, 2025 hadi Agosti, 2025 hivyo kutoa nafasi kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea na michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo ilisimama kupisha fainali hizo.
Bodi ya Ligi inatoa wito kwa klabu zote kuhakikisha zinaongeza nguvu katika maandalizi ya timu zao kiufundi pamoja na masuala mengine hasa yahusuyo miundombinu ya viwanja, ambavyo vitakaguliwa kabla ya kurejea kwa Ligi.
Viwanja na Maandalizi ya Timu
Viwanja vitakavyokosa sifa vitaondolewa katika orodha na klabu mwenyeji italazimika kuteua uwanja mwingine miongoni mwa vilivyothibitishwa kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani.
Bodi inazitakia kila la kheri klabu zote na wadau wengine katika maandalizi yao kuelekea kurejea kwa Ligi Kuu ya NBC.
Ratiba ya Michezo ya Ligi Kuu NBC Raundi ya 16 hadi 30
Raundi ya 16
1 Februari 2025
- Yanga vs Kagera Sugar – 16:00 – KMC Complex
2 Februari 2025 - Tabora United vs Simba – 16:00 – Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Raundi ya 17
5 Februari 2025
- Tabora United vs Namungo – 16:00 – Ali Hassan Mwinyi
- Yanga vs Kengold FC – 16:00 – KMC Complex
- Dodoma Jiji vs Pamba – 19:00 – Jamhuri Stadium
6 Februari 2025
- Tanzania Prisons vs Mashujaa – 14:00 – Sokoine Stadium
- Fountain Gate vs Simba – 16:15 – Tanzanite Kwaraa
- Azam vs KMC – 19:00 – Azam Complex
7 Februari 2025
- Coastal Union vs JKT Tanzania – 16:00 – Sheikh Amri Abeid
- Singida Black Stars vs Kagera Sugar – 16:00 – CCM Liti Stadium
Raundi ya 18
9 Februari 2025
- Pamba Jiji vs Azam – 16:00 – CCM Kirumba
- Namungo vs Dodoma Jiji – 19:00 – Majaliwa Stadium
10 Februari 2025
- Kengold vs Fountain Gate – 16:00 – Sokoine Stadium
- KMC vs Singida Black Stars – 16:00 – KMC Complex
- JKT Tanzania vs Yanga – 16:00 – Meja Isamuhyo
11 Februari 2025
- Mashujaa vs Coastal Union – 16:00 – Lake Tanganyika Stadium
- Simba vs Tanzania Prisons – 16:00 – KMC Stadium
- Kagera United vs Tabora United – 19:00 – Sokoine Stadium
Raundi ya 19
14 Februari 2025
- Yanga vs Dodoma Jiji – 16:00 – KMC Complex
- Singida Black Stars vs Pamba Jiji – 16:00 – CCM Liti Stadium
15 Februari 2025
- Simba vs Mashujaa – 16:00 – Benjamin Mkapa
- Kagera Sugar vs Azam – 19:00 – Kaitaba Stadium
Raundi ya 20
18 Februari 2025
- JKT Tanzania vs Namungo – 16:00 – Meja Isamuhyo
- Fountain Gate vs KMC – 16:00 – Tanzanite Kwaraa
- Coastal Union vs Tabora United – 16:00 – Sheikh Amri Abeid
19 Februari 2025
- Dodoma Jiji vs Tanzania Prisons – 16:00 – Jamhuri Stadium
- Yanga vs Singida Black Stars – 19:00 – KMC Complex
Raundi ya 21
21 Februari 2025
- Tanzania Prisons vs Tabora United – 14:00 – Sokoine Stadium
- JKT Tanzania vs Kagera Sugar – 16:00 – Isamuhyo
22 Februari 2025
- Kengold vs KMC – 16:00 – Sokoine Stadium
- Dodoma Jiji vs Fountain Gate – 19:00 – Jamhuri Stadium
23 Februari 2025
- Singida Black Stars vs Pamba – 14:00 – CCM Liti
- Mashujaa vs Yanga – 16:00 – Lake Tanganyika Stadium
- Namungo vs Coastal Union – 19:00 – Majaliwa Stadium
24 Februari 2025
- Simba vs Azam – 16:00 – KMC Complex
Raundi ya 22
26 Februari 2025
- Fountain Gate vs Tanzania Prisons – 14:00 – Tanzanite Kwaraa
- Singida Black Stars vs Mashujaa – 16:00 – CCM Liti Stadium
- Kagera Sugar vs KMC – 19:00 – Kaitaba Stadium
27 Februari 2025
- JKT Tanzania vs Kengold – 16:00 – Isamuhyo
- Azam vs Namungo – 19:00 – Azam Complex
28 Februari 2025
- Tabora United vs Dodoma Jiji – 14:00 – Ali Hassan Mwinyi
- Pamba Jiji vs Yanga – 16:00 – CCM Kirumba Stadium
1 Machi 2025
- Coastal Union vs Simba – 16:00 – Sheikh Amri Stadium
Raundi ya 23
5 Machi 2025
- Kengold vs Mashujaa – 16:00 – Sokoine Stadium
6 Machi 2025
- KMC vs Fountain Gate – 16:00 – KMC Complex
- Namungo vs Singida Black Stars – 19:00 – Majaliwa Stadium
- Azam vs Tanzania Prisons – 21:00 – Azam Complex
7 Machi 2025
- Tabora United vs JKT Tanzania – 16:00 – Ali Hassan Mwinyi
- Kagera Sugar vs Pamba Jiji – 19:00 – Kaitaba
- Dodoma Jiji vs Coastal Union – 21:00 – Jamhuri Stadium
8 Machi 2025
- Yanga vs Simba – 19:15 – Benjamin Mkapa National Stadium
10 – 12 Machi 2025
- CRDB Federation Cup
17 – 26 Machi 2025
- FIFA International Window
Raundi ya 24
1 Aprili 2025
- Tabora United vs Yanga -16:00 – Ali Hassan Mwinyi
2 Aprili 2025
- Pamba Jiji vs Namungo – 14:00 – CCM Kirumba Stadium
- KMC vs Tanzania Prisons – 16:00 – KMC Complex
- Fountain Gate vs Singida Black Stars – 16:00 – Tanzanite Kwaraa Stadium
3 Aprili 2025
- JKT Tanzania vs Dodoma Jiji – 16:00 – Isamuhyo Stadium
- Kengold vs Azam – 16:00 – Sokoine Stadium
- Kagera Sugar vs Coastal Union – 19:00 – Kaitaba Stadium
2 Mei 2025
- Simba vs Mashujaa – 16:00 – KMC Complex
Raundi ya 25
5 Aprili 2025
- Pamba Jiji vs Tabora United – 14:00 – CCM Kirumba Stadium
- Mashujaa vs Fountain Gate – 16:00 – Lake Tanganyika Stadium
6 Aprili 2025
- Tanzania Prisons vs Kagera Sugar – 14:00 – Sokoine Stadium
- Singida Black Stars vs Azam – 16:00 – CCM Liti
- Dodoma Jiji vs Kengold – 18:30 – Jamhuri Stadium
- Namungo vs KMC – 21:00 – Majaliwa Stadium
7 Aprili 2025
- Yanga vs Coastal Union – 16:00 – KMC Complex
5 Mei 2025
- JKT Tanzania vs Simba – 16:00 – Isamuhyo
Raundi ya 26
8 Aprili 2025
- Pamba Jiji vs Fountain Gate – 16:00 – CCM Kirumba Stadium
9 Aprili 2025
- JKT Tanzania vs Namungo – 14:00 – Isamuhyo
- Kengold vs Tanzania Prisons – 16:00 – Sokoine Stadium
- Dodoma Jiji vs Kagera Sugar – 19:00 – Jamhuri Stadium
10 Aprili 2025
- Mashujaa vs Tabora United – 16:00 – Lake Tanganyika Stadium
- Coastal Union vs Singida Black Stars – 16:00 – Sheikh Amri Abeid Stadium
- Azam vs Yanga – 17:00 – Azam Complex
11 Mei 2025
- KMC vs Simba – 16:00 – KMC Complex
11 – 13 Mei 2025
- CRDB Bank Federation Cup Quarter Finals
18 – 20 Mei 2025
- CAF Semi Finals
Raundi ya 27
18 Aprili 2025
- Tanzania Prisons vs JKT Tanzania – 16:00 – Sokoine Stadium
- KMC vs Dodoma Jiji – 16:00 – Sokoine Stadium
19 Aprili 2025
- Singida Black Stars vs Tabora United – 16:00 – CCM Liti Stadium
- Kagera Sugar vs Azam – 19:00 – Kaitaba Stadium
20 Aprili 2025
- Fountain Gate vs Yanga – 16:00 – Tanzanite Kwaraa Stadium
- Namungo vs Mashujaa – 19:00 – Majaliwa Stadium
21 Aprili 2025
- Coastal Union vs Kengold – 16:00 – Sheikh Amri Abeid Stadium
8 Mei 2025
- Simba vs Pamba Jiji – 16:00 – CCM Kirumba Stadium
Raundi ya 28
12 Mei 2025
- Tanzania Prisons vs Coastal Union – 16:00 – Sokoine Stadium
- Kagera Sugar vs Mashujaa – 18:30 – Kaitaba Stadium
13 Mei 2025
- Kengold vs Pamba Jiji – 16:00 – Sokoine Stadium
- JKT Tanzania vs Fountain Gate – 14:00 – Isamuhyo Stadium
- Azam vs Dodoma Jiji – 19:00 – Azam Complex
- Yanga vs Namungo – 16:00 – KMC Complex
14 Mei 2025
- Simba vs Singida Black Stars – 16:00 – KMC Complex
- Tabora United vs KMC – 16:00 – Sokoine Stadium
Raundi ya 29
21 Mei 2025
- Michezo yote itaanza *1600 Hours* katika viwanja mbalimbali
Raundi ya 30
25 Mei 2025
- Michezo yote itaanza *1600 Hours* katika viwanja mbalimbali
Hii ni ratiba rasmi ya Ligi Kuu NBC Tanzania 2024-2025 raundi ya pili.
Michezo ya Kusisimua ya Raundi ya 20 hadi 25
Kipindi cha katikati ya msimu kinatarajiwa kuwa na michezo ya kusisimua, hususan katika raundi ya 20 hadi 25, ambapo timu zenye ushindani mkubwa kama Yanga, Simba, Azam, na Namungo zitakutana. Mashabiki wanashauriwa kufuatilia kwa karibu ratiba hizi ili wasikose ladha ya burudani ya soka la Tanzania.
Raundi ya 26 hadi 30: Hatua za Mwisho za Ligi
Katika raundi za mwisho, timu zitajitahidi kukusanya alama muhimu ili kuepuka kushuka daraja au kubeba taji la ubingwa. Yanga na Simba, kwa kawaida, ndizo timu zinazopigiwa chapuo, lakini timu kama Azam, KMC, na Singida Black Stars zinaweza kutoa changamoto kubwa.
Mchezo wa Kariakoo Derby
- 8 Machi 2025: Yanga vs Simba, Saa 1:15 Usiku – Benjamin Mkapa National Stadium
Kariakoo Derby ni moja ya michezo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini na nje ya mipaka.
Hitimisho
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inatoa wito kwa mashabiki, wachezaji na klabu zote kujiandaa kwa ratiba mpya iliyotolewa. Hakika huu ni msimu wa kipekee na unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali zaidi.
Ligi Kuu NBC msimu wa 2024-2025 inaahidi kuwa yenye msisimko na ushindani mkubwa. Klabu zote zinapaswa kujipanga vyema ili kufikia malengo yao. Bodi ya Ligi inawatakia klabu zote kila la kheri katika msimu huu.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Tazama Hapa Makundi ya AFCON 2025
2. Orodha ya Mabingwa Kombe la Shirikisho Afrika
3. Orodha Ya Mabingwa Klabu Bingwa Afrika
4. Wafungaji Bora Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025
5. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025