Orodha ya Kambi za JKT Tanzania
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Orodha ya Kambi za JKT Tanzania,kambi za JKT, Habari mwana Habarika24, karibu katika makala hii ambayo itaenda kukuonyesha kambi zote za JKT na katika mikoa zinazopatikanaKama wewe ni muhitimu wa kidato cha sita na unatarajia kujiunga na mafunzo ya JKT ya muda mfupi basi haina budi ukafahamu kambi mbali mbali za JKT zitakazotumika kwa ajiari ya mafunzo hayo.
Hapa tutaenda kukuonyesha kambi zote za JKT ambazo zinatumika katika kutoa mafunzo kwa vijana na mikoa zinakopatikana.
Kuhusu JKT
Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1963. Jeshi la Kujenga Taifa au kwa kifupi JKT, liliundwa ili kuponya majeraha yaliyoachwa na serikali ya kikoloni miongoni mwa jamii ya watanzania ambayo ni pamoja na ubaguzi miongoni mwao katika misingi ya kidini, makabila, rangi na kipato. Chombo hiki ni muhimu katika kuelimisha na kuandaa vijana wa kitanzania kiuzalendo, kimaadili, kinidhamu na kuwafanya raia wema wanaopenda kutumikia na kulinda nchi yao.
Vikosi vya JKT ni mahali ambapo vijana hupata fursa ya kujifunza kikamilifu na kwa vitendo, maana na umuhimu wa kazi na pia kujifunza kutoa huduma kwa Taifa lao bila kutegemea kulipwa ujira wowote. Kwa hiyo, imedhihirika wazi ya kuwa wajibu wa JKT katika maendeleo ya Taifa hili ni mkubwa na muhimu sana.
Nchi mbalimbali duniani zina taasisi zinazofanana na taasisi yetu ya JKT. Kwa msingi huo nchi yetu kuwa na JKT ni jambo la kujivunia sana. JKT vilevile ni chombo cha kujenga Umoja na Utaifa kwa vijana wetu.
Orodha ya Kambi za JKT Tanzania
Kambi za JKT
Kambi za JKT ni maeneo tengefu yaliyoko chini ya usimamizi wa jeshi l kujenga taifa JKT amablo huyatumia ili kutoa mafunzo kwa vijana. Mafunzo yanayotolewa kwa vijana kupitia JKT hutolwa kwa mujibu wa sheria na vijana mara baada ya kubangiwa kambi zo wanatakiwa kulipoti mara moja.
Kupitia kambi za mafunzo ya JKT vijana hupewa mafunzo ambayo;
- Huwafunza stadi za maisha,
- Huwaengea uzalendo
- kuimarisha umoja wa kitaifa

Orodha ya Kambi za JKT na Mikoa Zinakopatikana
Hapa chini tunaenda kukuwekea kambi zinazotoa mafunzo ya JKT Tanzania
Kambi za Mafunzo Ya JKT na Mikoa Yake | |
Jina la Kambi | Mkoa |
JKT Bulombola | Kigoma |
JKT Rwamkoma | Mara |
JKT Msange | Tabora |
JKT Kanembwa | Kibondo-Kigoma |
JKT Mtabila | Kasulu-Kigoma |
JKT Mpwapwa | Dodoma |
JKT KibitI | Pwani |
JKT Mgulani | Dar Es Salaam |
JKT Ruvu | Pwani |
JKT Oljoro | Arusha |
JKT Makutupora | Dodoma |
JKT Mgambo | Tanga |
JKT Mbweni | Dar Es Salaam |
JKT Chita | Morogoro |
JKT Maramba | Tanga |
JKT Makuyuni | Arusha |
JKT Mafinga | Iringa |
JKT Mlale | Songea-Ruvuma |
JKT Nachingwea | Lindi |
JKT Itende | Mbeya |
JKT Itaka | Songwe |
JKT Luwa | Sumbawanga-Rukwa |
JKT Milundikwa | Sumbawanga-Rukwa |
Jinsi ya Kujiunga na Kambiza Mfunzo za JKT
Ifahamike kuwa kama unahitaji kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa JKT, Basi jeshi hili kila mwaka hutoa tangazo la nafasi za kujiunga na mafunzo ya jeshi na ili kujiunga lazima uweze kupitia baadhi ya michakato kama vile
- Kujaza form za maombi
- Kusubili majibu ya maombi
- Kujiunga na kambi uliyopangiwa
- Kuhudhulia mafunzo ya JKT
Vitu Muhimu vya Kua Navyo Unapoenda Kujiunga Na Kambi
- Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni, iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
- T-shirt ya rangi ya kijani
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
- Shuka za rangi ya blue bahari.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Track suit ya rangi ya kijani au blue.
- Hati muhimu zitakazotumika wakati wa Udahili wa Kujiunga na E limu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vya Kuhitimu kidato cha Nne
- Fedha ya ziada.
Faida za Mafunzo yatolewayo Na kambi za JKT

Kambi za JKT hutumika kutoa mafunzo kwa vijana ambayo huwa na faida nyingi sana kwa vijana wenyewe pamoja na Taifa kwa ujumla wake, hapa tumekuwekea baadhi ya faida za mafunzo yatolewayo katika kambi za JKT
- Kuimarisha Uzalendo na Nidhamu
- Kukuza Ujuzi na Stadi za Maisha
- Kuandaa Jeshi la Akiba
- Kutoa Ajira na Uzoefu kwa Vijana.
- Kutoa Elimu ya Kujitegemea
- Kushiriki katika Shughuli za Maendeleo ya Jamii
- Kutoa Msaada Wakati wa Maafa na Dharura
Majukumu Ya Msingi
1. Malezi ya Vijana
- Vijana kufundishwa moyo wa kupendana bila kujali tofauti za itikadi, dini, kabila na kipato.
- Kupenda kazi za mikono.
- Kuthamini na kuendeleza mila, desturi na kudumisha utamaduni wa Taifa.
- Kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.
2. Ulinzi wa Taifa
- Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
- Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.
3. Uzalishaji Mali
- Ili kuwafanya vijana wa kitanzania waepukane na kusumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKT linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKT. Uzalishaji mali unaofanywa na JKT ni pamoja na:-
- Kujenga na kukarabati majengo
- Viwanda na Kilimo
- Madini na Nishati
- Utalii
- Ulinzi kwa Taasisi binafsi (Security Guard Services)
- Maduka (Super Market)
- Kuunganisha magari na mitambo
- Huduma za elimu
Hitimisho
Mafunzo nanayotolewa na kambi ya JKT ni mafunzo muhimu sana kwa ujenzi wa taifa imala na lenye umoja. Pia mafunzo haya yanawafanya vijana kua wakakamavu katika nyanja ya uzalishaji kufanya kazi ya aina yoyoyte na katika mazingira ya aina yoyote.
Kama hukua na utambuzi juu ya kambi za mafunzo ya JKT na mikoa yake naamini ya kua makala hii itakua imekupa mwongozo wa kutosha. Kama unaswali au ushauli wowote basi usiache kuweka komenti yako hapa chini kwenye uwanja wa komenti.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Ratiba ya Mechi Za Leo Ligi Mbali Mbali Duniani
2. Ratiba Ya Ligi Kuu England 2024/2025 EPL
3. Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025
4. JINSI ya Kupata TIN Number Online
5. Jinsi Ya Kuangalia usajili wa kampuni BRELA
6. Fomu ya Kujiunga na Usalama Wa Taifa Tanzania
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku