Njinsi ya Kuweza Kutazama Channel za Azam Tv Bure, Njia ya kuangalia channels za Azam Tv Bure, Kutazama Azam Tv kupitia simu, Habari, karibu kwenye mwongozo wa namna ya kuangalia channels za Azam Tv bure.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Kama ulisha wahi kufikilia kutazama Azam Tv na hukuweza kutokana na gharama zake basi katika makala hii tutaenda kukuonyesha njia rahisi ya kuweza kutazama channel za Azam Tv buree kupitia simu yako ya mkononi (Simu janja)
Njinsi ya Kuweza Kutazama Channel za Azam Tv Bure
Azam Tv ni miongoni mwa makampuni makubwa zaidi nchini Tanzania kwa utoaji wa huduma ya urushaji wa channels za runinga kwa kutumia visimbuzi vyake. Azam Tv ina visimbuzi vya aina mbili ambavyo ni
- Visimbuzi vya Athena
- Visimbuzi vya Dishi
Visimbuzi hivi na kampuni kwa ujumla wake imekua maarufu zaidi kutokana na aina ya channel zinazorushwa kwenye visimbuzi vyake. Ili kufahamu channel zilizopo kwenye visimbuzi vya Azam Tv bonyeza HAPA
Njia ya kuangalia channels za Azam Tv Bure
Hata kama huna kisimbuzi cha Azam Tv jua ya kua unaweza kutazama channel mbalimbali zilizopo kwenye Azam Tv. Ili kuweza kutazama channel za Azam Tv hata kama huna kisimbuzi basi unaweza kufuata hatua zifuatazo.
1. Pakua App ya Azam Max
- Nenda play store na upakue application ya Azam Max na uinstall kwenye simu yako
2. Jisajili
- Baada ya kupakua App ya Azam Max ifungue na uweze kutengeneza Akaunti yako, kwa kujaza taarifa muhimu kwa kufuata maelekezo yatakayokua yanaonekana kwenye skrini yako.
Njinsi ya Kuangalia Channels
Baada ya kupakua App ya Azam Max na kuweza kuinstall kwenye simu yako sasa unawez kufurahia channel za Azam Tv bure kabisa kupitia simu yako. Kuweza kutazama channel za Azam Tv bure embu fuata hatua hizi hapa chini;
1. Chukua simu yako na ufungue App ya Azam Tv
2. Ingia kwenye Akaunti yako ya Azam TV
3. Nenda kwneye orodha ya channels za Azam Tv
4. Bonyeza channel unayotaka kuangalia
5. Furahia vipindi vya channel ya Azam Tv
– Kumbuka ili kuweza kuangalia channels za Azam Tv kupitia Azam Max lazima simu yako iwe imeunganishwa na huduma ya internet na pia weka akilini kwamba App ya Azam Max haisuport matumiz ya Wif.
– Channel za bure unazoweza kuangalia kupitia Azam Max nizile za ndani ya nchi kama vile
- Channel za habari na jamii, ITV,TBC, STAR TV, Channel Ten nk.
- Channel za Dini ksm Arise and Shine Tv n.k
Ili kutazama channel nyingine itakupasa kufanya malipo kulingana na aina ya channels unazaotaka kuzitazama.
Faida ya Kutumia Azam Max
Kunafaida nyingi sana kwa mpenzi wa Azam Tv kuweza kutumia Azam Max App. Hapa chini ni miongoni mwa faida za kutumia App ya Azam Max.
- Kufurahia channels za bure kutoka Azam Tv
- Gharama nafuu, kwani kutumia Azam Max utahitaji Mb kidogo tu
- Kutazama Channel za Azam Tv mahari popote pale na wakati wowote
Hitimisho
Ili uweze kufurahia channele zitolewazo na Azam Tv basi fahamu kua ni rahisi zaidi ukiwa na Azam Max App ya Azam Tv inayopatikana playstore na inakupa uhuru wa kutizama channels za Azam Tv bure wakati wowote na mahari popote kwa gharama nafuu sana.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Orodha ya Channel Zote za Visimbuzi Vya Azam TV
2. Orodha ya App Nzuri za Kuangalia Mpira Live Kwenye Simu
3. Jinsi Ya Kukata Tiketi Ya Basi Mtandaoni
4. Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania
5. Bei ya Vifurushi vya Azam TV Kisimbuzi Cha Dishi Na Antena