Nafsi 51 za Kazi Kutoka MDA’s & LGA’s March 2025
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali pamoja na Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MDA’s & LGA’s) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 51 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili
MASHARTI YA JUMLA.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
• Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
• Computer Certificate
• Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
vi. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 07 Aprili, 2025
xii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Bonyeza HAPA kupakua PDF File ya Tangazo lote
Kwa Matagazo ya Ajira Mpya Kila Siku Bonyeza HAPA.