NAFASI za Kazi WINBILL Supermarket
Jina la Kampuni: WinBill Supermarket
Mahali: Mbezi Temboni
Nafasi ya Kazi: Mhasibu wa Fedha
Maelezo ya Kazi
-
Usimamizi wa Fedha Taslimu: Kujumuisha kufanya malipo kwa wasambazaji, kupokea fedha kutoka kwa makashia mwisho wa zamu zao, kutoa float kwa makashia, kushughulikia petty cash kuu ya supermarket, kusimamia mahitaji ya malipo na kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kutosha kulipa wasambazaji inapohitajika.
-
Usimamizi wa Miashara ya Benki: Kuhakikisha mauzo ya kila siku ya fedha taslimu yanawekwa benki siku inayofuata ya kazi, kufanya upatanisho wa akaunti za benki mara kwa mara pamoja na cash count reconciliations.
-
Usimamizi wa Hesabu za Mali (Inventory): Kuhakikisha mizunguko ya bidhaa kutoka dukani inalingana na taarifa kwenye mfumo, kufuatilia bidhaa zilizoharibika au kuisha muda wa matumizi.
-
Uzalishaji wa Bakery: Kufuatilia mizunguko ya malighafi na kuchambua tija inayopatikana kutokana na malighafi zilizopatikana.
-
Usimamizi wa Mali Zisizohamishika (Fixed Assets): Kuhakikisha mali zisizohamishika za kampuni zimesajiliwa na kusimamiwa ipasavyo kwenye fixed asset register.
-
Usimamizi wa Wasambazaji: Kuhifadhi taarifa za wasambazaji wanaosambaza kwa mkopo na kufuatilia masharti ya mikopo.
-
Uzingatiaji wa Sheria na Kanuni: Kuhakikisha kampuni inafuata matakwa ya kisheria kama vile PAYE, WCF, NSSF, Kodi ya Kampuni, SDL, VAT, pamoja na kanuni maalumu kwa supermarkets na bakeries.
-
Utoaji wa Taarifa za Fedha: Kuhakikisha miamala yote inaingizwa kwenye accounting package kwa wakati, kuchambua taarifa na kutoa ripoti za kifedha kila mara zitakapohitajika na wakurugenzi.
-
Ukaguzi wa Ndani na Nje: Kushirikiana na wakaguzi wa ndani na nje na kuhakikisha kampuni inapata ripoti safi.
-
Nafasi ya Uongozi: Kuchukua jukumu la usimamizi pale meneja anapokosekana ili kuhakikisha shughuli za dukani zinaendelea vizuri na kutoa msaada wa kitaalamu pale inapohitajika.
Sifa za Mwombaji
-
Awe mhudumu aliyehitimu kutoka taasisi/chuo kinachotambulika nchini Tanzania; CPA itakuwa ni faida ya ziada.
-
Awe tayari kufanya kazi kwa muda mrefu.
-
Uzoefu wa angalau miaka 3; uzoefu katika sekta hii utapewa kipaumbele.
-
Awe tayari kuanza kazi mara moja baada ya kupangiwa.
-
Mkazi wa Kimara au Mbezi atapewa kipaumbele.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Tuma maombi kwa:
WinBill Enterprises Limited
S.L.P. 11621, Dar es Salaam
Kwa barua pepe: [email protected]
Mwisho wa kutuma maombi: 3 Septemba 2025
Kumbuka: Uwe tayari kuitwa kwenye usaili kwa muda mfupi baada ya mwisho wa kutuma maombi.