Nafasi za kazi Msaidizi Wa Ufugaji Nyuki Daraja La II Nafasi 47 August 2024
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara zinazo jitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Elfu sita, mia mbili, hamsini na saba (6,257) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili
MSAIDIZI WA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING ASSISTANT
II) NAFASI 47
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusimamia manzuki;
ii. Kutunza hifadhi za nyuki;
iii. Kukusanya takwimu za ufugaji nyuki;
iv. Kutunza kumbukumbu za kazi za utafiti;
v. Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo;
vi. Kutoa leseni za biashara za mazao ya nyuki;
vii. Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na matumizi bora ya mazao ya nyuki; na
viii. Kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada ya UfugajiNyuki kutoka Vyuo vinavotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B