Nafasi za kazi Mpima Ardhi Daraja La II Kutoka MDAs na LGAs – Nafasi 4 August 2024
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara zinazo jitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Elfu sita, mia mbili, hamsini na saba (6,257) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili
MPIMA ARDHI DARAJA LA II (LAND SURVEYOR II) – NAFASI 4
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuingiza taarifa za Upimaji (alpha numeric data) kwenye kompyuta;
ii. Kukagua kazi za upimaji na kuingiza taarifa za kazi zilizothibitishwa kwenye
komputa;
iii. Kufanya upimaji picha (aerial triangulation and block adjustment);
iv. Kusimamia na kuchukua vipimo vya “tide gauges”; na
v. Kupima Ardhi katika Serikali za Mitaa.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu/Shahada katika fani ya Upimaji Ardhi kutoka Chuo
Kikuu cha Ardhi au Taasisi yoyote inayotambuliwa na “National Council of Professional
Surveyors” (NCPS).
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E