Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga June 2025
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 ya tarehe 29 Aprili, 2025. Hivyo; anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo;-
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II NAFASI (4)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada au NTA level 6 katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu, kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, na mwenye ujuzi wa Kompyuta.
MAJUKUMU YA KAZI KWA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
i. Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register)
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register)
iii. Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
iv. Kupokea majalada yanayotoka kwa watendaji
v. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi (file tracking)
vi. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga nyaraka za taasisi katika majalada kulingana na somo husika (classification indexing)
vii. Kupanga na kudhibiti nyaraka katika vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu (repositories).
viii. Kuhudumia na kuwasimamia watafiti katika chumba cha utafiti.
ix. Kurudisha majalada yaliyosomwa kwenye ghala la kuhifadhia nyaraka. Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, 20Barabara ya Mwanza, 37182 Chamaguha, S.L.P.28, Shinyanga. Simu: 028-2763213, Barua pepe: [email protected], tovuti: www.shinyangamc.go.tz
MASHARTI YA KAZI
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali na ajira ya kudumu (TGS, C1)
DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 10)
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe na Lessen ya Daraja la C au E ya uendeshaji wa magari ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha
VETA au NIT au Chuo kinachotambulika na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA DARAJA LA II
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (Logbook)
vi. Kufanya usafi wa gari.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali na Ajira ya Kudumu (TGS B1).
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
ii. Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina
ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika. Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, 20Barabara ya Mwanza, 37182 Chamaguha, S.L.P.28, Shinyanga. Simu: 028-2763213, Barua pepe: [email protected], tovuti: www.shinyangamc.go.tz
iii. Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,” Statement of Results”,” Provisional Results” au” Transcripts HAVITAKUBALIKA.
iv. Kwa Waombaji waliosoma nje ya Nchi, Elimu ya Kidato cha Nne au Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
v. Kwa waombaji waliosoma Vyuo nje ya Nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
vi. Waombaji watakokidhi sifa zinazotakiwa ndio watakaoitwa katika usaili.
vii. Barua ya maombi iliyosainiwa na Mwombaji inaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
viii. Waombaji wenye mahitaji maalum (special needs/disability) wanatakiwa kuainisha kwenye maombi yao.
ix. Waombaji watakaowasilisha Taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba. isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
xi. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 13 Juni, 2025.
xii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
xiii. Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.