Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi March 2025
Ajira

Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi March 2025

Kisiwa24By Kisiwa24March 27, 2025No Comments3 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi March 2025

Kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupata kibali cha ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.228/613/01F/064 cha tarehe 13 Machi, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Ikungi anatangaza nafasi ya kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye Sifa za kujaza nafasi kama ilivyoorodheshwa kwenye Tangazo hili.

MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – (NAFASI 1)

SlFA ZA MWOMBAJI:

Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na aliyefuzu mafunzo ya  Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6.Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
ii. Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa;
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Divisheni/Kitengo/Sehemu husika;
vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; na
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

NGAZI YA MSHAHARA:

Mshahara wa kuanzia ni kima cha serikali katika ngazi ya TGS. C kwa mwezi.

MASHARTI YA JUMLA:

i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na mwenye umri usiopungua Miaka Kumi na Nane (18) na usiozidi miaka Arobaini na Tano (45). Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

ii. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili

iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika

iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma,maelezo,nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate, – vyeti vya kitaaluma (professional Certificate from respective boards)

v. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU/NACTE na NECTA)

vi. “Testimonials”, Provisional Results, Statement of Results, Hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CAC45//257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi

ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria

x. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 06 Aprili 2025.

xi. MUHIMU kumbuka kuambatanisha Barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, Anuani ya Barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI,
S.L.P 42,
SINGIDA.

ix. Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia Anuani ifuatayo http://portal.ajira.go.tz, Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.

Bonyeza Hapa Kupakua Tangazo Lote

Kwa matangazo ya Ajira Mpya Kila siku Bonyeza HAPA

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleNafasi 6 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa March 2025
Next Article Nafasi 57 za Kazi Taasisi Mbalimbali za Umma March 2025
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
  • NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited
  • NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania
  • NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • NAFASI za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025780 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025442 Views

NAFASI Mpya 5476 za Mafunzo ya Ufundi Stadi Katika Fani Mbalimbali

December 6, 2025423 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.