TAMISEMI: FORM FIVE SELECTION 2025/2026

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Geita June 2025

Filed in Nafasi Za Kazi Tanzania 2025 by on June 3, 2025 0 Comments

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA.97/228/01A/25 cha
terehe 29/04/2025. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa nafasi tisa (09) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Geita June 2025

DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 09)

KAZI NA MAJUKUMU

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
ii. Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
vi. Kufanya usafi wa gari.

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA.

NGAZI YA MSHAHARA

Ngazi ya Mshahara ni TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 16 Juni, 2025.

MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *