Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»NAFASI za Kazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza June 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza June 2025

Kisiwa24By Kisiwa24June 7, 2025No Comments5 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza amepokea kibali cha ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/228/01/A/25 ya tarehe 29 April, 2025. Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kwa watanzania wote wenye sifa kujaza nafasi zifuatazo:-

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza June 2025

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II -NAFASI NNE (4).

MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II

1. Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye regista (Incoming Correspondence Register)
II. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Corespondence Register)
III. Kusambaza majalada kwa Watendaji (Action Officers)
IV. Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa Watendaji (Action Officers)
V. Kutafuta Kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji
VI. Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali pengine yanapo hifadhiwa.
VII. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)

SIFA ZA KUAJIRIWA

1. Awe na elimu ya Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI)
II. Awe na Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
III. Awe na ujuzi wa kutumia Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS C

DEREVA DARAJA LA II -NAFASI TANO (5)

MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II

1. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
II. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
III. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
IV. Kufanya na kusambaza nyaraka mbalimbali pale inapohitajika.
V.Kujaza na kutunza taarifa za safari katika daftari la safari.
VI.Kufanya usafi wa gari na
VII. Kazi zingine atakazopangiwa na Mwajiri.

SIFA ZA KUAJIRIWA

I. Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au kidato cha sita (VI) mwenye Leseni ya Udereva Daraja ‘E’ au C’ ya uendeshaji.
I1. Awe na cheti/vyeti kilichokupa Daraja la leseni ya Udereva ulilonalo.
III. Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila ya kusababisha ajali.
IV. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basi Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya (VETA) au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS B

DEREVA WA MITAMBO DARAJA LA II – NAFASI MOJA (1).

MAJUKUMU YA DEREVA WA MITAMBO DARAJA LA II

1. Kuendesha mitambo kikamilifu bila kusimamiwa.
II. Kuweka vipimo mbalimbali vinavyotakiwa kufuatana na kazi anayofanya na jinsi anavyoelekezwa na kiongozi wa kazi hiyo.
III. Kutoa huduma ya kwanza ya matengenezo ya mitambo na pia aweze kutoa maelekezo sahihi ya ubovu wa mitambo anapotakiwa kufanya hivyo.
IV. Kuandika vizuri ‘log sheet’ na kuweka kumbukumbu sahihi ya matumizi ya vifaa kwa mfano mafuta, grisi na vipuri.
V. Kuhakikisha kuwa mashine/mitambo inatumika kwa kazi zinazotakiwa.
VI. Kufanya usafi wa mtambo.
VII. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA KUAJIRIWA

1. Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV).
II. Awe na leseni Daraja ‘G’ ya uendeshaji mitambo pamoja na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo. Awe na cheti/vyeti kilichokupa Daraja la leseni ya udereva ulilonalo.
IV. Awe na uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu (300) au miezi mitatu (3) bila kusababisha ajali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGOS A.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.

i. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira na ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretariati ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.

Maombi yote yaambatane na vivuli (photocopies) vya vyeti vya Elimu na Taaluma, ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, Cheti cha Kuzaliwa, Picha mbili (02) (Pasport size) za rangi za hivi karibuni.
iv. Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae), yenye anuani na namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua pepe (E-mail addres) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika..
V. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NAСТЕ)
vi. Maombi yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
vii. Waombaji waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
X.”Testimonial” “Posvisional Results” “Statement of Results” hati ya matokeo ya kidato cha nne au sita (Form IV and Form VI) Results Slips”.HAVIRUHUSIWI katika maombi ya nafasi hizi.
xi. Waombaji ambao watakuwa na utofauti wa majina wanatakiwa kuambatanisha DEED POOL iliyotolewa na kusainiwa na Msajili wa Hati na Viapo kutoka Wizara
ya Aridhi.
хii. Awe na kitambulisho cha uraia (NIDA).
xiii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 19 June, 2025.

  • BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleOrodha ya App 69 Za Mikopo Zilizofungiwa na Bot
Next Article VIWANGO vya Mishahara ya Watumishi Serikali 2025 (TGS salary Scale)
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
  • NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited
  • NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania
  • NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • NAFASI za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025783 Views

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

July 12, 2025543 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025445 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.