NAFASI za Internship Mpenja TV & Mpenja Film
Mpenja TV ni kituo maarufu cha mtandaoni kinachojihusisha na kuripoti habari za michezo, hususan soka, ndani na nje ya Tanzania. Kituo hiki kinamilikiwa na Salum Mpenja, ambaye ni mwandishi mashuhuri wa habari za michezo. Kupitia mitandao ya kijamii kama YouTube, Facebook, na Instagram, Mpenja TV huwapa watazamaji taarifa za papo kwa papo, mahojiano na wachezaji, tathmini za mechi, na uchambuzi wa kina unaovutia wapenzi wa soka kote nchini. Uwazi, uharaka wa taarifa na ubunifu wa maudhui vimeifanya Mpenja TV kuwa chaguo la wengi wanaotaka kufuatilia burudani ya michezo kwa njia ya kisasa.
Kwa upande mwingine, Mpenja Film ni mradi wa kisanaa unaolenga kutangaza vipaji vya waigizaji chipukizi wa Kitanzania kupitia filamu za kizalendo. Mradi huu umejikita katika utayarishaji wa filamu fupi na tamthilia zinazogusa maisha ya kila siku ya Watanzania, zikiwa na mafunzo na burudani kwa wakati mmoja. Mpenja Film inalenga kuinua sekta ya filamu nchini kwa kutumia teknolojia ya kisasa, huku ikitoa fursa kwa vijana kujifunza na kushiriki katika tasnia ya uigizaji. Kwa kupitia jukwaa hili, Salum Mpenja anaendelea kuonesha kuwa yeye si mwandishi wa michezo tu, bali pia ni mzalendo anayehamasisha maendeleo ya sanaa na utamaduni wa Kitanzania.
NAFASI za Internship Mpenja TV & Mpenja Film
Ili kuweza kusoma nafasi za internship, vigezo na njia ya kutuma maombi tafadhari bonyeza linki hapo chini
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO