Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
JIUNGE NA WHATSAPP CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA WHATSAPP GROUP LETU HAPA,
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI (03)
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuorodhesha barua zinazoingia masijala mwenye regista (Incoming Correspondence Register)
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing CorrespondenceRegister)
iii. Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
iv. Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji
v. Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji
vi. Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa.
vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi
miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini – Serikalini.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
“Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
iv. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na wanasheria/Wakili.
v. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
vi. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
vii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
viii. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika.
ix. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
x. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
xi. Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agosti, 2024.
xiv. MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,
S.L.P 9596,
ORKESUMET.
xv. Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”
xvi. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKILIWA
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikanaMkwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
xiv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.