Close Menu

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    What's Hot

    NAFASI Za Kazi Geita Gold Mine (GGM)

    November 16, 2025

    NAFASI za Kazi Halmashauri Mbalimbali Tanzania 2025

    November 16, 2025

    Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) November 2025

    November 16, 2025
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Kisiwa24
    • Home
    • Ajira
    • Makala
    • Michezo
    • Usaili
    • Kuitwa Kazini
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Kisiwa24
    Home » Nafasi Mpya 29 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe
    Ajira

    Nafasi Mpya 29 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe

    Kisiwa24By Kisiwa24July 24, 2024No Comments6 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

    Nafasi Mpya 29 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe

    Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga

    BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA TELEGRAM CHANNEL YETU
    BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA WHATSAPP CHANNEL YETU

    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada nne (04) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –

    Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe (Mwisho Wa Maombi 26 Julai 2024)

    MATANGAZO YA AJIRA BOFYA HAPA

    MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II NAFASI 03

    KAZI NA MAJUKUMU

    1. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
    2. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
    3. Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
    4. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
    5. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika idara/kitengo/sehemu husika.
    6. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
    7. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
    8. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama
    vile Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

    MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II NAFASI 03

    KAZI NA MAJUKUMU

    1. Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence regisster)
    2. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register)
    3. Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
    4. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji
    5. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajika na watendaji.
    6. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa Kumbukumbu/nyaraka.
    7. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
    8. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
    9. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
    10. Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
    11. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa Kompyuta.

    MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (“Village Executive”) NAFASI – 20

    KAZI NA MAJUKUMU

    1. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
    2. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji,
    3. Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo katika Kijiji
    4. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
    5. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
    6. Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
    7. Mwenyekiti wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
    8. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
    9. Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji
    10. Kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
    11. Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na;
    12. Kuwajibika kwa Mtendaji wa Kata.

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti au NTA level 5 katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

    DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 03

    KAZI NA MAJUKUMU

    1. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
    2. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
    3. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
    4. Kufanya kusambaza nyaraka mbalimbali.
    5. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari na
    6. Kufanya Usafi wa Gari.
    7. Kufanya kazi nyingine kadri atavyoelekezwa na msimamizi wake.

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha Nne (IV) Awe na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (01) bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.

    MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

    1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
    2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
    3. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Carriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
    4. “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
    5. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
    6. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
    7. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
    8. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
    9. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
    10. Waombaji walisoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
    11. Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
    12. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
    13. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 26 Julai, 2024

    MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa

    • Mkurugenzi Mtendaji,
    •  Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe,
    •  S.L.P 01,
    •  Mbogwe.

    JINSI YA KUTUMA MAOMBI

    Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”

    Soma Pia:

    ✓Nafasi Mpya 25 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe

    ✓Nafasi Mpya za Kazi Almashauri ya Wilaya ya Kibiti Julai, 2024

    ✓Nafasi za Kazi Mtendaji Wakijiji III Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama – Posti 5

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Kisiwa24
    • Website

    Related Posts

    NAFASI Za Kazi Geita Gold Mine (GGM)

    November 16, 2025

    NAFASI za Kazi Halmashauri Mbalimbali Tanzania 2025

    November 16, 2025

    Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) November 2025

    November 16, 2025
    Leave A Reply Cancel Reply

    Demo
    Top Posts

    Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    November 14, 2025944 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

    July 12, 2025879 Views

    PDF ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025/2026

    September 30, 2025696 Views
    Stay In Touch
    • Facebook
    • YouTube
    • TikTok
    • WhatsApp
    • Twitter
    • Instagram
    Latest Reviews

    Subscribe to Updates

    Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

    Demo
    Covid-19 Statistics

    [rb_covid countries_code=’CN’ countries_label=’China’ columns=1]

    Most Popular

    Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

    November 14, 2025944 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

    July 12, 2025879 Views

    PDF ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Magereza 2025/2026

    September 30, 2025696 Views
    Our Picks

    NAFASI Za Kazi Geita Gold Mine (GGM)

    November 16, 2025

    NAFASI za Kazi Halmashauri Mbalimbali Tanzania 2025

    November 16, 2025

    Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) November 2025

    November 16, 2025

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    • Home
    • Buy Now
    © 2025 ThemeSphere. Designed by ThemeSphere.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.