Nafasi Mpya 17 Za Kazi Kutoka Halmashauri ya Mji Kondoa
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Mji Kondoa kuomba nafasi za kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea Kibali chenye Kumb. Na. FA 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 05)
KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
ii. Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari ( log book)
vi. Kufanya usafi wa gari
vii. Utajaza taarifa za utendaji kazi kila wiki kwenye Mfumo wa ess (PEPMIS)
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria
mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PF FILE
MACHAGUZI YA MHARIRI;
1. Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Agosti 2024 (UDOM)
2. Nafasi Mpya Za Kazi Wizara ya Maji Agosti 2024
3. Nafasi Mpya 4 Za Kazi Kutoka Chuo kikuu cha Mzumbe Agosti 2024
4. Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Agosti 2024
5. Tangazo La Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali Za Umma Agosti 2024
6. Nafasi Mpya 18 Za Kazi Kutoka Halmashauri Ya Wilaya Ya Tunduru Agosti 2024
7. Nafasi Mpya 18 Za Kazi Kutoka Halmashauri Ya Mji Kasulu Agosti 2024