Nafasi Mpya 15 Za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Ya Tabora
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Mkurugenzi wa Manispaa amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi.
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini – Serikalini.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
iv. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
v. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
vi. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katikakada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
vii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
viii. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
ix. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
x. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
xi. Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Septemba, 2024.
xiv. MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
BONYEZA HAPA KUPAKUA FILE NZIMA
Mapendekezo Ya Mhariri;
1. Nafasi Mbali Mbali Za kazi zilizotangazwa Agosti 2024
2. Nafasi Mpya Za Kzi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala
3. Nafasi Mpya 27 Za Kazi Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa
4. Nafasi Mpya Za Kazi Kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru
5. Nafasi Mpya 10 Za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
6. Nafasi Mpya Za Kazi Kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Agosti 2024
7. Nafasi Mpya 17 Za Kazi Kutoka Halmashauri ya Mji Kondoa
8. Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Agosti 2024