NAFASI 70 za Kazi ya Udereva Kutoka Unitrans Tanzania Limited September 2025
Unitrans Tanzania Limited
Unitrans Tanzania Limited inakaribisha maombi kutoka kwa waombaji waliokidhi vigezo na wenye ujuzi ili kujaza nafasi zifuatazo:
Dereva wa Malori – Nafasi 70 (Unitrans Tanzania)
Eneo la Kazi: Kilombero
Aina ya Mkataba: Msimu (Seasonal)
Majukumu
-
Kusafirisha miwa kutoka mashambani hadi kiwandani.
-
Kufanya kazi zingine zinazohusiana na taaluma ya udereva kama utakavyopangiwa.
Sifa za Mwombaji
-
Awe na uelewa wa sheria na kanuni za usalama barabarani.
-
Awe na leseni ya udereva daraja E.
-
Awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
-
Awe na cheti halali cha uendeshaji wa malori makubwa (Rigid au HGV-Pulling Trucks) kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
-
Awe na uzoefu wa angalau miaka 2 wa kuendesha malori.
-
Awe na umri kati ya miaka 25 na 45.
-
Awe tayari kufanya kazi usiku.
-
Awe na barua halali ya uthibitisho wa leseni kutoka Jeshi la Polisi Tanzania.
Jinsi ya Kuomba
Maombi yatumiwe kwa:
Meneja wa Rasilimali Watu
Unitrans Tanzania Ltd
S.L.P 50, Kidatu
Waombaji wanapaswa kuambatanisha nyaraka zifuatazo kwenye maombi yao:
-
Barua ya maombi
-
Wasifu binafsi (Curriculum Vitae – CV)
-
Nakala za vyeti husika
-
Nakala ya cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)
-
Nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)
Maombi yatumiwe kwa barua pepe kupitia:
[email protected]
Mwisho wa kutuma maombi: Septemba 30, 2025
Taarifa ya Faragha ya Takwimu
Kwa kutuma maombi kwa nafasi hii, mwombaji anakubali kuwa taarifa zake binafsi zitahifadhiwa na kutumika na kampuni kwa madhumuni ya mchakato wa ajira pekee, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Leave a Reply