Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Utumishi Wa Umma 2027

December 20, 2025

Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Sheria Ngazi Ya Cheti 2027

December 20, 2025

Orodha ya Tahasusi za Kidato cha Tano 2027

December 20, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»Nafasi 6 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Nyang`Hwale May 2025
Ajira

Nafasi 6 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Nyang`Hwale May 2025

Kisiwa24By Kisiwa24May 30, 2025No Comments4 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA. 97/228/01/A/25
cha tarehe 29.04.2025. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada mbili (02) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –

Nafasi 6 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Nyang`Hwale May 2025

MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (“Office Management Secretary II” NAFASI 04)

 KAZI NA MAJUKUMU

i. Kuchapa barua,taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
ii. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao , na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
iii. Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio ,miadi, wageni ,tarehe za vikao,safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
vi. Kukusanya ,kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne au sita wenye Stashahada(Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha ,wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile:Word,Excel ,Powerpoint ,internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS C

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (“Records Management Assistant II”NAFASI 02)

KAZI NA MAJUKUMU

i. Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register)
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register)
iii. Kusambaza ,majalada kwa watendaji (action officers)
iv. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
v. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
vi. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
vii. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
viii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi(file tracking)
ix. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliehitimu mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ,wenye ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

1 Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.

2 Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.

3 Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

4 Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).

5 Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

6 Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).

7 Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. 8 Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

9 Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

10 Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

11 Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Juni, 2025.

  • BONYEZA HAPA KUPAKUA PDF FILE

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleCV ya Feisal Salum Abdallah (Fei Toto)
Next Article Nafasi 15 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Biharamulo May 2025
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Utumishi Wa Umma 2027
  • Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Sheria Ngazi Ya Cheti 2027
  • Orodha ya Tahasusi za Kidato cha Tano 2027
  • Sifa Za Kujiunga Kidato Cha Tano Tanzania (Cutting point form 5) 2026/2027
  • Sifa Za Kujiunga Na Kozi Ya Pharmacy 2027

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2027

December 20, 20251,260 Views

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025788 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025446 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.