NAFASI 526 za Kazi Kutoka UTUMISHI July 2025
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni taasisi ya serikali ya Tanzania iliyoanzishwa kwa lengo la kurahisisha na kuboresha mchakato wa ajira kwa watumishi wa umma. Sekretarieti hii hufanya kazi kwa niaba ya waajiri wa umma kwa kutangaza nafasi za kazi, kupokea na kuchambua maombi ya kazi, kufanya usaili na hatimaye kuwasilisha majina ya waliofanikiwa kwa waajiri husika. Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa ajira za serikali zinapatikana kwa uwazi, usawa na kwa kuzingatia sifa za waombaji bila upendeleo.
PSRS inafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu na utendaji bora ili kuhakikisha kuwa sekta ya umma inapata rasilimali watu wenye uwezo, ujuzi na maadili yanayohitajika katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Kupitia tovuti yake rasmi na vyombo vya habari mbalimbali, Sekretarieti ya Ajira huendelea kutoa matangazo ya nafasi mpya za kazi, kutoa maelekezo kwa waombaji na pia kuchapisha matokeo ya usaili. Hii imeifanya kuwa kiungo muhimu kati ya raia wanaotafuta ajira na serikali inayohitaji watumishi wenye weledi.
NAFASI 526 za Kazi Kutoka UTUMISHI July 2025
Kwa niaba ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Afrika, Mweka (CAWM), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Taasisi ya Mipango ya Maendeleo ya Vijijini (IRDP), Kituo cha Teknolojia ya Magari Tanzania (TATC), Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE), Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inawaalika Watanzania mahiri na wenye sifa stahiki kujaza nafasi za ajira mia tano ishirini na sita (526) zilizoorodheshwa hapa chini.
Ili kuweza kusoma nafasi zilizopo, vigezo na njia ya kutuma maombi tafdhari bonyeza linki hapo chini