Nafasi 50 za Kazi Kada ya Afya March 2025
Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna mifumo miwili mikuu ya utawala inayojulikana kama MDAs (Ministries, Departments, and Agencies) na LGAs (Local Government Authorities).
MDAs (Wizara, Idara, na Wakala): Hizi ni taasisi za serikali kuu zinazohusika na uundaji wa sera, usimamizi wa rasilimali, na utoaji wa huduma kwa ngazi ya kitaifa. MDAs zinajumuisha wizara mbalimbali kama vile Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, pamoja na idara na wakala zinazojitegemea zinazotekeleza majukumu maalum ya serikali.
LGAs (Mamlaka za Serikali za Mitaa): Hizi ni mamlaka zinazofanya kazi katika ngazi ya mkoa, wilaya, manispaa, miji, na vijiji. LGAs zinawajibika kwa utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maji, na maendeleo ya miundombinu. Mfano wa LGA ni Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, ambayo ina wajibu wa kusimamia maendeleo na huduma ndani ya manispaa hiyo.
Ushirikiano kati ya MDAs na LGAs ni muhimu katika kuhakikisha maendeleo ya taifa na utoaji bora wa huduma kwa wananchi. MDAs huunda sera na kutoa miongozo, wakati LGAs hutekeleza sera hizo kwa kuzingatia mahitaji ya jamii katika maeneo yao husika.
MSAIDIZI WA AFYA (HEALTH ASSISTANT) NAFASI – 50
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuchukua Sampuli za Maji na Chakula na kuzipeleka kwa afisa afya mazingira au afisa afya mazingira msaidizi
ii. Kutambua na kuweka kumbukumbu ya vyanzo vya maji
iii. Kuandaa ramani ya maeneo yenye uchafuzi wa maji ili kuchukua hatua zinazotakiwa
iv. Kushirikiana na kamati za maji za vijiji, na mitaa katika kuhakikisha usalama wa vyanzo vya maji
v. Kuhamasisha jamii kulinda vyanzo vya maji
vi. Kuhamasisha jamii kujenga na kutumia vyoo bora
vii. Kusaidia kuuelimisha jamii kuhusu tabia njema za usafi
viii. Kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa kwa mkuu wake kazi
ix. Kuhamasisha jamii kubuni, kupanga, kutekeleza na kusimamia mipango shirikishi jamii ya afya ya mazingira
x. Kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba
xi. Kufanya ukaguzi wa nyumba za kuishi na biashara
xii. Udhibiti wa taka hatari zikiwamo taka zitokanazo na huduma za afya
xiii. Kusimamia sheria ndogondo za afya mazingira na;
xiv. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha mafunzo ya Msaidizi wa Afya kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali TGHS – A