Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»NAFASI 17 za Kazi Muleba District Council
Ajira

NAFASI 17 za Kazi Muleba District Council

Kisiwa24By Kisiwa24July 6, 2025No Comments6 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amepokea kibali cha Ajira mpya kwa Ikama ya mwaka 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-

NAFASI 17 za Kazi Muleba District Council

DEREVA II – NAFASI 09

MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA II
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali pale inapohitajika.
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
vi. Kufanya usafi wa gari
vii. Kazi nyingine anazopangiwa na mwajiri.

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B

MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 01

MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
ii. Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
vi. Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
ix. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au Kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word,
Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS C

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 05

KAZI NA MAJUKUMU

i. Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming correspondence register)
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register)
iii. Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers)
iv. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji.
v. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji.
vi. Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C

MSAIDIZI WA MAENDELEO YA JAMII II – NAFASI 02

KAZI NA MAJUKUMU

i. Kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia Jinsia
ii. Kuraghabisha jamii kuanzia ngazi ya familia katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathimini mipango na/au mradi yao ya maendeleo
iii. Kuhamasisha kuondokana na mila/desturi potofu na kuwa na mtazamo wa kupenda mabadiliko
iv. Kutoa taarifa za utekelezaji wa kazi zake kila mwezi
v. Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia
vi. Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi
vii. Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa za matukio mbalimbali k.m vifo milipuko ya magonjwa, masoko, uzalishaji mali, vyakula, ajira na unyanyasaji wa kijinsia
viii. Kuhamasisha jamii kujiunga na Elimu ya Watu Wazima
ix. Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya Watoto
x. Kukusanya, kuchambua na kuweka takwimu zinazozingatia jinsia zitakazowezesha jamii kupanga mipango yao.
xi. Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe na Cheti cha kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Buhare na Rungemba au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate
from Respective Boards).
v. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19 Julai2025.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleNAFASI 4 za Kazi Watu Creadit July 2025
Next Article AUDIO: Tannah Ft Moni Centrozone – YOLO | Download
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
  • NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited
  • NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania
  • NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • NAFASI za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025783 Views

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

July 12, 2025718 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025445 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.