Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»Nafasi 15 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Biharamulo May 2025
Ajira

Nafasi 15 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Biharamulo May 2025

Kisiwa24By Kisiwa24May 30, 2025No Comments4 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo amepokea kibali cha utekelezaji wa Ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha terehe 29 Aprili, 2025. Hivyo, anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo kutuma maombi kwa nafasi zifuatazo:-

Nafasi 15 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Biharamulo May 2025

MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 05

MAJUKUMU YA KAZI.

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri
ii. Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
iii. Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara / Kitengo Sehemu husika.
vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI.

• Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).

• Awe na cheti cha Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA LEVEL 6 ya Uhazili kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali / vyuo vya Utumishi wa Umma (Uhazili)
• Awe amefaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dk 1
• Awe na ujuzi wa kutumia program za computer za ofisi kama vile Word, Excel, Power Point. E- mail na Publisher.

NGAZI YA MSHAHARA – TGS C

DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 06

KAZI NA MAJUKUMU YA UDEREVA.

• Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
• Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
• Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
• Kukusanya na kusambaza nyaraka mbali mbali.
• Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
• Kufanya usafi wa gari.
• Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI.

• Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV).
• Awe na Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
• Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic driving course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinacho tambuliwa na Serkali.

NGAZI YA MSHAHARA TGS B

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 04

MAJUKU YA KAZI.

• Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka/Majalada yanayohitajika na wasomaji.
• Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa Kumbukumbu/ Nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwaajili ya matumizi ya Ofisi.
• Kuweka/kupanga Kumbukumbu, Nyaraka katika Reki (File racks/cabinets) katika Masjala/Vyumba vya kuhifadhia Kumbukumbu.
• Kuweka Kumbukumbu (Barua,Nyaraka nk.) katika Majalada.
• Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka Taasisi za Serkali.

SIFA ZA MWOMBAJI.

• Awe na Elimu ya kidato cha Nne IV au VI.
• Awe na cheti cha Stashahada (Technician certificate- NTA LEVEL 6) cha Utunzaji wa Kumbukumbu katika mojawapo ya Fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.

NGAZI YA MSHAHARA TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA MWOMBAJI

i. Mwombaji awe ni raia wa Tanzania na mwenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waanishe kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Secretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Mwombaji aambatanishe nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
iv. Mwombaji aambatanishe Nakala ya Kitambulisho cha Uraia au Namba ya Kitambulisho hicho kutoka mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo binafsi (CV) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya Barua pepe pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wakuaminika ambao siyo ndugu,nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofika kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa.
vi. Picha moja Passport size iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (Statement of Results havitakubalika).
viii.Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe kazi na wanapaswa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 06/06/2025.
xii. MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa

  • BONYEZA HAPA KUPAKUA TANGAZO LOTE

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleNafasi 6 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Nyang`Hwale May 2025
Next Article Nafasi 8 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngara May 2025
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
  • NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited
  • NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania
  • NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • NAFASI za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

July 12, 20251,178 Views

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025788 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025446 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.