Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Shule za Sekondari za Advanced (Form 5 & 6) Mkoa wa Arusha

December 23, 2025

NAFASI Za Kazi World Vision Tanzania

December 21, 2025

NAFASI Za Kazi Standard Bank Group

December 21, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»NAFASI 12 za Kazi Misungwi District council July 2025
Ajira

NAFASI 12 za Kazi Misungwi District council July 2025

Kisiwa24By Kisiwa24July 5, 2025No Comments4 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wialaya ya Misungwi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2024/2025 chenye Kumb.Na FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji
Mbulu anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-

NAFASI 12 za Kazi Misungwi District council July 2025

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI NNE (04)

MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuorodhesha barua zinazoingia masijala mwenye regista (Incoming Correspondence Register)
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing CorrespondenceRegister)
iii. Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
iv. Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji
v. Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/FillingCabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa.
vi. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI.

Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

DEREVA DARAJA LA II NAFASI NANE (08)

MAJUKUMU YA KAZI

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
iv. Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote,
v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
vi. Kufanya usafi wa Gari,
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali

MAELEKEZO YA JUMLA.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E- mail Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
v. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Julai, 2025

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleMakato ya Kutoa Pesa kwenye ATM za NMB
Next Article NAFASI za Kazi Bukombe District council July 2025
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

NAFASI Za Kazi World Vision Tanzania

December 21, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi Standard Bank Group

December 21, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Yas Tanzania

December 21, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • Shule za Sekondari za Advanced (Form 5 & 6) Mkoa wa Arusha
  • NAFASI Za Kazi World Vision Tanzania
  • NAFASI Za Kazi Standard Bank Group
  • NAFASI za Kazi Yas Tanzania
  • Sifa za Kujiunga na Chuo Cha University of Dar es salaam Computing Center (UCC)

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

December 21, 20252,313 Views

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025798 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025453 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.