NAFASI 11 za Kazi Rungwe District Council September 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Rungwe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na moja (11) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
MASHARTI YA JUMLA KWA MUOMBAJI
i. Waombaji wote wawe raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates – Cheti cha
mtihani wa Kidato cha IV na VI – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards)
v. Waombaji watakaowasilisha “Testmonial” “Provisioinal Result”,”Statement of result”, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vi. Wapombaji waliosoma nje Nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA NA NACTE).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji wa kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja ‘E’ au ‘C’ wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya; S. L. P 148, Tukuyu, Simu: +2552552693, Nukushi +2552552586, Barua pepe: [email protected], Tovuti: [email protected]
x. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 01 Oktoba, 2025
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO
Leave a Reply