Msimamo Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/2025 , UEFA Champions League Standing 2024/2025, Habari mwana Kisiwa24 Blog karibu katika makala hii fupi ya kimichezo ambayo kwa kina itaenda kuangazia juu ya msimamo wa ligi ya Mabingwa Ulaya inayofahamika kama UEFA Champions League. Kama wewe ni shabi wa soka basi sina shaka kua lazima utakua miongoni mwa mamilioni ya wapenda soka wanaofuatilia michuano hii ya EUFA Champions League kwa msimu huu wa 2024/2025.
Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa Champions League) inayojulikana kwa kifupi cha UCL yaliyo anzishwa mnamo mwaka 1955, haya ni mashindano yanayofanyika kila mwaka kwa kushirikisha virabu vya mpira wa miguu katika bala la Ulaya (UEFA). Hujumuisha timu zilizoshiliki zilizo maliza katika nafasi za juu katika ligi za mataifa mbalimbali balani ulaya.
Msimamo Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024/2025
Msimu mpya wa 2024/2025 wa UEFA Champions League umesha anza kutimua mbio zake huku tuki shuhudia vilabu zaidi ya 35 kutoka mataifa mbalimbali barani ulaya yakichuana uwanjani kuwania ubingwa huu wenye thamani zaidi Duniani na ulaya kwa ujumla. Msimu huu mpya wa mashindano ya UEFA Champions League umekua wa tofauti sana na mwapenda soka wameshuhudia mabadiliko makubwa zaidi katika muundo wa uendeshaji wake ukilinganisha na miaka ya hapo awaili. Hapa katika kurasa hii utapata ufafanuzi wa mabadiliko hayo ikiwa pamoja na msimamo wa ligi ya Mabingwa Ulaya kama ijulikanavyo na walio wengi UEFA Champions League Standing.
Muundo wa UEFA Champions League 2024/2025
Kuanza kwa msimu huu mpya wa mashindani ya ligi ya mabingwa ulaya (Uefa Champions League) kumekua na mabadiliko makubwa ya kimfumo, muundo na uendeshaji Pia kumekua na mabadiliko ya idadi ya timu zinazoshiriki. Kwa mwaka huu kumekua na timu 36 amabo zitacheza kwa mfumo wa ligi ukilinganisha na hapo awali kulikua na timu 32 tu ambazo ziliweza kucheza kwa mfumo wa makundi ya timu 4 kwa makundi 8 ili kufuzu robo fainali, nusu fainali hadi kufikia fainali.
Hatua ya Ligi
Kwenye hatua hii timu 36 zitacheza kwa mfumo wa ligi na kufuzu kundelea kutakua kwenye mfumo ufuatao
1. Baada ya mshindano kukamilika timu zitakazo maliza katika msimamo wa 1,2,3,4,5,6,7 na 8 zitafuzu moja kwa moja kwenda katika hatua ya mtoano ya 16 bora
2. Kwa timu zitakazo maliza hatua hii zikiwa katika nafasi ya 9 hadi 24 zitaingia kwenye hatua ya mtoano (play off) ili kutafuta timu nane zitakazoenda kwenye hatua ya 16 bora kuungana na timu 8 zilizofuzu moja kwa moja.
3. Na timu zitakazo maliza msimamo kwa kushika nafasi ya 25 hadi ile ya 36 zitaondolewa kwenye mashindano.
Kwa msimu huu mpya wa UEFA Champions League timu zitakazoondolewa katika michuano baada ya msimamo hazita ruhusiwa kwenda kwenye mashindano yale ya Europa League au UEFA Conference League bali zitaaga kabisa mashindano.
Muundo wa Hatua ya Mtoano , Robo Fainali na Fainali za UEFA Champions League 2o24/2025
Baada ya mechi za ligi kukamilika na zile za mtoano za play off timu 16 zilizoweza kufuzu zitaingia katika hatua ya mtoano ili kusaka tiketi ya kuingia katika hatua ya robo fainali, katika hatua hii mfumo wa uendesahji utaendela kama ulivyokua hapo awali hadi kupata timu 2 zitakazocheza fainali.
Msimamo UEFA Champions League 2024/2025
Hapa chini ni msimamo wa ligi ya mabingwa barani ulaya kwa msimu wa 2024/2025;
Rank | Club | MP | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Liverpool | 7 | 7 | 0 | 0 | 15 | 2 | 13 | 21 |
2 | Barcelona | 7 | 6 | 0 | 1 | 26 | 11 | 15 | 18 |
3 | Arsenal | 7 | 5 | 1 | 1 | 14 | 2 | 12 | 16 |
4 | Inter | 7 | 5 | 1 | 1 | 8 | 1 | 7 | 16 |
5 | Atlético Madrid | 7 | 5 | 0 | 2 | 16 | 11 | 5 | 15 |
6 | Milan | 7 | 5 | 0 | 2 | 13 | 9 | 4 | 15 |
7 | Atalanta | 7 | 4 | 2 | 1 | 18 | 4 | 14 | 14 |
8 | Leverkusen | 7 | 4 | 1 | 2 | 13 | 7 | 6 | 13 |
9 | Aston Villa | 7 | 4 | 1 | 2 | 9 | 4 | 5 | 13 |
10 | Monaco | 7 | 4 | 1 | 2 | 13 | 10 | 3 | 13 |
11 | Feyenoord | 7 | 4 | 1 | 2 | 17 | 15 | 2 | 13 |
12 | LOSC | 7 | 4 | 1 | 2 | 11 | 9 | 2 | 13 |
13 | Brest | 7 | 4 | 1 | 2 | 10 | 8 | 2 | 13 |
14 | Dortmund | 7 | 4 | 0 | 3 | 19 | 11 | 8 | 12 |
15 | Bayern | 7 | 4 | 0 | 3 | 17 | 11 | 6 | 12 |
16 | Real Madrid | 7 | 4 | 0 | 3 | 17 | 12 | 5 | 12 |
17 | Juventus | 7 | 3 | 3 | 1 | 9 | 5 | 4 | 12 |
18 | Celtic | 7 | 3 | 3 | 1 | 11 | 10 | 1 | 12 |
19 | PSV | 7 | 3 | 2 | 2 | 13 | 10 | 3 | 11 |
20 | Club Brugge | 7 | 3 | 2 | 2 | 6 | 8 | -2 | 11 |
21 | Benfica | 7 | 3 | 1 | 3 | 14 | 12 | 2 | 10 |
22 | PSG | 7 | 3 | 1 | 3 | 10 | 8 | 2 | 10 |
23 | Sporting | 7 | 3 | 1 | 3 | 12 | 11 | 1 | 10 |
24 | VfB Stuttgart | 7 | 3 | 1 | 3 | 12 | 13 | -1 | 10 |
25 | Man City | 7 | 2 | 2 | 3 | 15 | 13 | 2 | 8 |
26 | Dinamo Zagreb | 7 | 2 | 2 | 3 | 10 | 18 | -8 | 8 |
27 | Shakhtar Donetsk | 7 | 2 | 1 | 4 | 7 | 13 | -6 | 7 |
28 | Bologna | 7 | 1 | 2 | 4 | 3 | 8 | -5 | 5 |
29 | Sparta Praha | 7 | 1 | 1 | 5 | 7 | 19 | -12 | 4 |
30 | RB Leipzig | 7 | 1 | 0 | 6 | 8 | 14 | -6 | 3 |
31 | Girona | 7 | 1 | 0 | 6 | 4 | 11 | -7 | 3 |
32 | Crvena zvezda | 7 | 1 | 0 | 6 | 12 | 22 | -10 | 3 |
33 | SK Sturm Graz | 7 | 1 | 0 | 6 | 4 | 14 | -10 | 3 |
34 | RB Salzburg | 7 | 1 | 0 | 6 | 4 | 23 | -19 | 3 |
35 | Slovan Bratislava | 7 | 0 | 0 | 7 | 6 | 24 | -18 | 0 |
36 | Young Boys | 7 | 0 | 0 | 7 | 3 | 23 | -20 | 0 |
Hitimisho
Huu umekua ni muundo mpya wa uendeshaji wa Ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA Champions League 2024/2025), Hivyo basi mashabiki walio wengi wanatamani kuona jinsi michuano hi itakavyoenda. Hadi sasa. Hadi sasa ni kwa jinsi msimamo ulivyo ni matumaini kwa mashabiki wa soka kutoka Uingereza kwani timu zao zinafanya vizuri huku msimamo ukiongozwa na klabu ya Liverpool,a Arsenal ikiwa katika nafasi ya 3 na Aston Villa ikiwa katika nafasi ya 9, hali si nzuri sana kwa klabu ya Man City kwani iko katika nafasi ya 25.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2025
2. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2025
3. Ratiba ya Mechi za Liverpool Ligi Kuu ya Uingereza EPL 2024/2025
4. Msimamo Wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 Tanzania Bara
5. Msimamo wa Ligi Kuu Uingereza EPL 2024/2025
6. Ratiba Ya Ligi Kuu England 2024/2025 (EPL Fixtures 2024/2025)