PDF: MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili wa Mahojiano TAMISEMI
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji waliowasilisha maombi ya ajira ya Mkataba wa nafasi ya Afisa
Lishe mwezi Mei, 2025 kuwa mchakato wa uchambuzi umekamilika.
Hivyo waombaji wote waliokidhi vigezo. wanatakiwa kushiriki katika usaili (Oral interview) kwa njia ya mtandao (live zoom). Usaili huu umepangwa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 8 Julai, 2025 kuanzia saa 4:00 asubuhi. Wasailiwa wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
1. Usaili utafanyika kwa tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu ambapo usaili utafanyika ni mahali alipo mwombaji kwa njia ya zoom.
2. Kila msailiwa anatakiwa kuandaa kompyuta mpakato/tablet au Ipad pamoja na kifurushi cha Internet kumwezesha kushiriki katika usaili kupitia zoom.
3. Wasailiwa wanatakiwa kuzingatia muda aliopangwa kuanza usaili.
4. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao dakika tano kabla ya muda aliopangiwa kuanza usaili.
NB: Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili wa Mahojiano TAMISEMI
Ili kuweza kusoma majina tafadhari bonyeza linki hapo chini ilinkupakua PDF ya majina
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA