MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Temeke Municipal Council September 2025

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Temeke Municipal Council September 2025

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Temeke Municipal Council September 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote
walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 15-09-2025 hadi 18-09-2025 na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye
usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo
usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV,
Kidato cha VI, Astashahada, Stashahada.
6. Wasailiwa kada ya Dereva watatakiwa kuja na Leseni ya Udereva ambayo haijaisha muda.
7. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form IV/VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
8. Kila Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
9. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
10. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).
11. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika.
12. Wasailiwa kada ya Dereva watatakiwa kuja na cheti kilichowapatia sifa ya daraja C au E kutoka
Chuo cha Usafirishaji NIT au Chuo kingine kilichoainishwa, baada ya kufuzu Mafunzo ya
Udereva.
13. Kwa wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana kwenye Cheti cha kuzaliwa, NIDA na Vyeti vya
taaluma watatakiwa kuja na DEEP POLL kutoka kwa Kamishina wa Ardhi.
14. Wasailiwa ambao majina yanatofautiana herufi watatakiwa kuja na Kiapo cha majina (Affidavit)
15. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

BONYEZZA HAPA KUDOWNOAD PDF YA MAJINA

error: Content is protected !!