MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Kinondoni Municipal Council September 2025
Mkurugenzi wa Manispaa katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa
kuendeshwa kuanzia tarehe 12-09-2025 hadi 13-09-2025 a hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI ambavyo ni: Cheti cha kuzaliwa, Cheti cha Kidato cha IV (Form Four), Cheti cha Mafunzo ya Mafunzo ya Msingi ya Uendeshaji
Madereva (Basic Driving Course), Cheti cha Mafunzo ya Leseni Daraja C ama E kutegemeana na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wakumbuke kuja na Leseni daraja C au E hai kama ilivyoainishwa kwenye Tangazo la Kazi
13. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA
Leave a Reply