MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Dar es Salaam City Council September 2025
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam anapenda kuwataarifu wasailiwa
walioongezwa kwa awamu ya pili Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa
kuendeshwa kuanzia tarehe tarehe 14/09/2025 hadi 18/09/2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi
waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia
maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo
usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti
vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
13. Waombaji ambao wanautofauti wa herufi katika kitambulisho cha Taifa na vyeti vya Taaluma kidato
cha Nne na cha Sita na Cheti cha kuzaliwa waje na kiapo (Affirdavit)
14. Waombaji wenye utofauti wa majina katika kitambulisho cha Taifa na vyeti vya Taaluma kidato cha
NNe na cha Sita na Cheti cha kuzaliwa wanatakiwa kufika na kiapo cha majina (Deed Pool)
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA
Leave a Reply