PDF: MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha UDSM June 2025
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 13 hadi 16 Julai 2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI NA ”TRANSCRIPT”, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. KWA WAOMBAJI WALIOSOMA NJE YA TANZANIA WAHAKIKISHE WANAKUJA NA CHETI/VYETI VYAO VYENYE WAKIA (GPA) ULIO KOKOTOLEWA (CALCULATED) NA TCU KWA MFUMO WA TANZANIA (FIVE (5) POINTS GRADE SYSTEM).
11. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
12. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
13. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
14. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha kubadili Jina (Deed poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha UDSM June 2025
Ili kuona majina ya walioitwa kwenye usaili chuo kikuu cha Dar es Salaam tafdhari bonyeza linki hapo chini;