PDF Majina Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Zimamoto April 2025
BOFYA HAPA KUPATA PDF YA MAJINA YA USAILI JESHI LA ZIMAMOTO
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anapenda kuwatangazia vijana walioomba kuajiriwa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia mfumo wa kuajiri ZIMAMOTO (ajira.zimamoto.go.tz), Usaili utafanyika kuanzia tarehe 05 Aprili, 2025 hadi 17 Aprili, 2025 kuanzia saa 1:00 asubuhi kwa kila kikundi.
Waombaji walioomba kuajiriwa na elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 05 hadi 09 Aprili, 2025 saa 1:00 asubuhi katika mikoa waliyochagua wakati wa kutuma maombi yao.
Waombaji wenye Shahada ya Kwanza na fani mbalimbali usaili wao utafanyika katika Ukumbi wa Andengenye – Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dodoma kuanzia tarehe 14 Aprili hadi 17 Aprili, 2025 saa 1:00 asubuhi kwa kila kikundi.
Tafadhali kumbuka yafuatayo:
- Kila mtu anatakiwa kufika kwa usaili kwa tarehe na muda uliopangwa na si vinginevyo.
- Kuwa nadhifu na kuvaa nguo za heshima.
Fika na vyeti halisi vyote vilivyotumika katika maombi ya ajira kama vile kidato cha nne, kidato cha sita, cheti cha ufundi stadi, cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho wa taifa (NIDA) - Kwa wale wanaoomba nafasi ya Udereva, pamoja na maelekezo haya, wanatakiwa kuleta leseni halisi ya Daraja E.
- Gharama za usafiri, chakula na malazi ni juu ya mhojiwa kwa muda wote atakaokuwa kwenye usaili.
Vijana watakaofanyiwa usaili katika Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wazingatie tarehe zao za usaili. Kwa kuongeza, mtu yeyote anayekuja kwa tarehe isiyopangwa hatakubaliwa.
Orodha ya Vijana waliochaguliwa kwa mahojiano pamoja na vikundi inapatikana katika tangazo hili kupitia PDF Hapa chini:
PDF YA MAJINA YA WAOMBAJI WENYE ELIMU YA KIDATO CHA NNE
PDF YA MAJINA YA WAOMBAJI WENYE SHAHADA
Imetolewa na;
Kamishna Jenerali
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu Dodoma
30 Machi, 2025