Majina Mapya ya Walioitwa Kazini 2025 – Utumishi na Ajira Portal, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetoa orodha ya majina ya watu walioitwa kazini kwa mwaka 2025 kupitia mfumo rasmi wa ajira. Hati hii muhimu ipo katika muundo wa PDF na inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa waombaji wote waliowahi kuwasilisha maombi ya nafasi za kazi serikalini.
Kuhusu UTUMISHI (PSRS)
PSRS ni chombo cha serikali kilichopewa jukumu la kuratibu na kusimamia mchakato mzima wa ajira katika sekta ya umma. Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 ya mwaka 2002, iliyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, PSRS imepewa mamlaka ya:
- Kutafuta na kuhifadhi kumbukumbu za wataalamu wenye ujuzi maalumu kwa ajili ya nafasi za ajira.
- Kusajili wahitimu na wataalamu kwa urahisi wa kujaza nafasi mbalimbali.
- Kutangaza nafasi za kazi zilizopo serikalini.
- Kuendesha mahojiano na kushirikisha wataalamu husika.
- Kushauri waajiri kuhusu masuala ya ajira.
- Kufanya majukumu mengine yoyote yanayoelekezwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma.

Umuhimu wa Wito wa Kazi UTUMISHI
Tangazo hili la kuitwa kazini linawahusu wale waliotuma maombi ya kazi katika sekta tofauti serikalini ikiwemo elimu, afya, ustawi wa jamii na nyanja nyingine. Ni hatua muhimu inayothibitisha kuwa mwombaji amefanikisha mchakato wa maombi, uchambuzi wa nyaraka, tathmini, na hatimaye uteuzi rasmi.
Jinsi ya Kuhakikisha Jina Lako Lipo
Ili kujua kama umechaguliwa, tembelea tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS). Hapo utapata orodha kamili ya majina yaliyotolewa kupitia tangazo la ajira 2025. Hakikisha unakagua jina lako na kuthibitisha uteuzi wako.
Wito huu wa ajira unaashiria fursa kubwa kwa Watanzania wanaotafuta ajira katika sekta ya umma. Kwa wale waliopata nafasi, ni mwanzo wa safari mpya ya kulitumikia taifa kupitia nyanja mbalimbali za kiutawala na kijamii.
Kwa urahisi wako, orodha ya majina pia imeambatanishwa ili kusaidia kuthibitisha uteuzi wa walioitwa kazini mwaka huu.
Kuhusu Sekretarieti ya Ajira (PSRS)
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali na hadhi ya Idara ya kujitegemea iliyoanzishwa hasa ili kuwezesha mchakato wa kuajiri wa wafanyakazi katika taasisi mbalimbali za Umma.
Maono ya Sekretarieti ya Ajira
- Maon yetu ni kuwa kituo cha ubora katika huduma ya umma kuajiri katika kanda.
Kazi Kuu za Sekretarieti ya Ajira (PSRS)
Kazi yetu kubwa ni Kufanya kuajiri watumishi wa umma kwa kutumia mbinu za kisasa kwa kuzingatia kanuni za usawa, uwazi na sifa na pia kutoa ushauri kwa waajiri juu ya maswala yanayohusiana na ajira.
- Kuajiri wafanyakazi kwenye taasisi za Umma,Jukumu kuu la PSRS ni kuwezesha kuajiri katika Huduma ya Umma.
- Kutafuta wataalamu mbalimbali wenye ujuzi maalum na kuandaa database kwa wataalamu hao kwa ajili ya kuajiri rahisi;
- Kurejista wahitimu na wataalamu kwa madhumuni ya urahisi wa rejea ya kujaza nafasi tupu;
- Kutangaza nafasi za kazi zinazotokea katika huduma ya umma;
- Kuhusisha wataalam husika kwa madhumuni ya kufanya mahojiano
- Kushauri waajiri juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na kuajiri, na
- Kufanya kitendo kingine chochote au kitu ambacho kinaweza kuelekezwa na Waziri anayehusika na Huduma ya Umma.
Utajuaje Kama Umeitwa Kazini Kupitia Utumishi
Kama ulifanya usaili kupitia utumishi na ajira portal basi unapaswa pia kufuatilia kujua kama ulichaguliwa kua miongoni mwa walioitwa kazini baada ya kufanya usaili. Sekretarieti ya Ajira (PSRS) hutoa PDF document ambayo huwa na majina ya walioitwa kazini baada ya kufaulu usaili wao. Document hizo hupatikana kupitia tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira (PSRS)
Hivyo basi ili kujua kama umeitwa kazi kupitia utumishi tembelea tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS).
Matangazo haya ya kuitwa kazini yanapatikana moja kwa moja kupitia tovuti rasmi ya sekretarieti ya Ajira (Utumishi). Pia hapa katika page hii utapata updates zote za majina ya waliotwa kazi utumishi leo, wiki hii, mwezi huu. ili kupata taarifa za sasa tafadhari tembelea ukrasa huu mara kwa mara.
MAWASILIANO Ya UTUMISHI
Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa mawasiliano yafuatayo;
Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
SLP 2320,
Dodoma.
+255 (26) 2963652












Leave a Reply