Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Tanga
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Tanga, Mbasi ya Dar to Tanga, Habari mwana Habrika24, niwakati mwingine tena napenda kukukaribisha katika makala hii ambayo itaenda kukupa maelekezo juu ya kampuni za mabasi ya Dar es Salaam kwenda Tanga.
Kama wewe ni miongoni mwa wasafiri ndani ya mkoa wa Dar na Tanga na bado hujafahamu ni kampuni zipi za mabasi zinazo fanya safari zake kati ya mkoa wa Dar es Salaam na Tanga basi jua ya kua makala hii fupi itakua na mwongo sahihi kwako kwani hapa tunaenda angazia baadhi ya kampuni za mabasi ambazo zinafanya safari zake nda ya mikoa ya Dar es Salaam na Tanga.

Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Tanga
Njia za Usafiri Kati ya Mkoa Wa Dar es Salaam na Tanga
Miko ya Dar na Tanga ipo katika mwambao wa pwani ya bahari ya Hindi hivyo kufanya njia za usafiri katika mikoa hii kua njia tatu ambazo ni;
- Njia ya Maji kupitia Baharini – Boti au Jahazi
- Njia ya Anga – Ndege
- Njia ya Aridhini – Gari
Hapa katika makala hii tutaenda kuangalia juu ya njia ya aridhini kwa kutumia mabasi.
Aina ya Mabasi Yanayofanya Safari zake Kati ya Dar es Salaam na Tanga
Kuna aina Tatu za mabasi yanayofanya safari zake baina ya mkoa wa Dar es Salaam na Tanga, Aina hizo zimewekwa katika madaraja kama vile;
- Mabasi ya daraja la kawaida – Ordinary class buses
- Mabasi ya daraja la kati – Semi Luuxury Buses
- Mabasi ya Draja la Juu – Luxury/ VIP Buses
Utofauti wa kimadaraja katika mabasi yanayofanya safari zake katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanaga huwekwa na huduma zinaztolewa katika mabasi hayo pindi yawapo safarini na ubora wa hadhi ya mabasi. Ubora wa kihadhi na huduma katika mabasi licha ya kuperekea madaraja lakini pia hupeleke kuwepo kwa utofauti katika gharama za nauli miongoni mwa mabasi hayo.
Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Tanga
Hapa chini tunaenda angazia baadhi ya kampuni za mabasi yanayokua yakifanya safari zake katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanga. Katika mikoa yote safari za mabasi na makampuni ya mabasi katika mkoa wa Dar kwenda Tanga ni Nyingi sana na hayana muda maalumu wa safari wakati wa mchana unaweza kwenda standi ya mabasi na ukapata usafiri.
1. Ratco express

2. Nacharo Royal Bus

3. Simba mtoto

4. Moud express

5. Raha leo express

6. Bembea

7. Dar express

8. Tashrif coach

Aina ya Huduma katika Mabasi Yanayofanya Safari zake Kati ya Dar na Tanga
Kumekua na safari nyingi sana za watu kati ya mkoa wa Dar na Tanga kiasi kwamba imepelekea kuwepo kwa kampuni nyingi sana zinazotoa huduma katika mikoa hii na hata kupeleka mabasi ya aina zote tatu yani ordinary class buses, Semi Luxury buses na hata Luxury buses, Hapa tunaenda kukutajia baadhi ya huduma zinazotolewa na basi ya daraja la kati na juu pindi yawapo safari iwe kutoka Dar kwenda Tanga au Tanga kwenda Dar.
- Huduma ya Kuchaji simu
- Huduma ya Kuangali TV
- Huduma ya Vinywaji na Vitafunwa
- Huduma ya Choo
Hitimisho
Nadhani kama ulikua hutambui aina ya kampuni za mabasi zinazofanya safari zake katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanga kupitia makala hii fupi utakua na uwelewa juu ya mabasi hayo hata ubora na huduma wanazotoa wanapokua safarini.
Hii itakusaidia kufanya maamuzi ni basi la daraja gani ungeweza kusafri nalo, lakini kumbuka ya kua huduma na hadhi ya basi katika daraja lake pia inapelekea kuongezeka kwa gharama za usafiri (Nauli) Mfano mabasi ya Daraja la juu nauli zake ni ghari sna ukilinganisha na zile za mabasi yaliko katika daraja la kawaida.
Hivyo basi kama ungependa kusafiri kistarehe na kifahari basi chaguo lako la kwanza litakua kwa mabsi yanayopatikana katika daraja la juu (Luxury) na kisha kwenya daraja la kati Semi Luxury lakini kama wewe unajali hasa kufika bila kuangalia chochote kile kwenye basi, basi chaguo la mabasi ya daraja la kawaida litakua namba moja kwako kwani hata bei zake za nauli ni nafuu ukilinganisha na zile za mabsi ya daraja la kati na juu.
Kama kuna kampuni yoyote ambayo tumeisahau na unaifahamu inafanya safari zake tai ya mkoa ea Dar es Salaam na Tanga basin usisite kuitaja hapo chini kwenye uwanja wa komenti ili kila mmoja wa abiria aweze kuongeza machaguo yake.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Mabasi Ya Dar es Salaam Kwenda Songea
2. Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Arusha
3. Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Mwanza
4. Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Tabora
5. Mabasi ya Dar es Salaam Kwenda Bukoba
6. Mabasi ya Dar Kwenda Mtwara
7. Jinsi Ya Kuangalia usajili wa kampuni BRELA
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku