MABADILIKO ya Eneo la Usaili Kada ya Mpiga Chapa Msaidizi Daraja II
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, anawajulisha waombaji kazi wa kada ya MPIGA CHAPA MSAIDIZI DARAJA II (ASSISTANT PRINTER II) kuwa kuna mabadiliko ya sehemu ya kufanyia usaili wa vitendo.
Usaili utafanyika Ofisi ya Mpiga chapa Mkuu wa Serikali (Idara ya kupiga chapa ya Serikali) -DAR ES SALAAM karibu na Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) badala ya Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) DODOMA. Aidha, Muda na tarehe unabaki kama ilivyokuwa kwenye tangazo la awali la kuitwa kwenye usaili