Katika mazingira ya sasa ya ajira nchini Tanzania, kupata ujuzi unaohitajika sokoni ni jambo la msingi kwa vijana wanaotafuta maisha bora. VETA (Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi) imeendelea kuwa nguzo muhimu kwa kutoa mafunzo ya vitendo yanayoandaa wahitimu kwa ajira au kujiajiri. Hapa chini tunakuletea listi ya kozi bora kabisa za VETA zenye ajira za uhakika kwa vijana wa Kitanzania.
Kozi za Ufundi Umeme (Electrical Installation)
Kozi hii inafundisha wanafunzi kuhusu ufungaji wa mfumo wa umeme majumbani na viwandani, ukarabati wa vifaa vya umeme, pamoja na usalama wa kazi za umeme. Katika dunia ya sasa ambapo ujenzi unaongezeka kila siku, mafundi wa umeme wanahitajika kwa wingi.
Faida za kuchukua kozi hii:
Ajira kwenye kampuni za ujenzi na viwanda
Kujiajiri kwa kufungua biashara ya umeme
Mafunzo kwa vitendo na vyeti vinavyotambulika kitaifa
Kozi ya Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)
Katika sekta ya usafirishaji, mafundi wa magari ni watu muhimu sana. VETA inatoa mafunzo kamili kuhusu matengenezo ya magari, vipuri, mfumo wa breki, mfumo wa mafuta na injini kwa ujumla.
Nini kinachovutia kwenye kozi hii:
Uhitaji mkubwa wa mafundi magari katika miji mikubwa
Uwezo wa kujiajiri kwa kufungua gereji binafsi
Mafunzo ya kisasa kwa kutumia magari ya kisasa
Kozi ya Useremala na Samani (Carpentry and Joinery)
Useremala ni mojawapo ya kozi ambazo zimekuwa na ajira endelevu kwa miongo mingi. Katika kozi hii, wanafunzi hujifunza kutengeneza samani kama meza, vitanda, makabati, milango na madirisha.
Fursa baada ya kuhitimu:
Kuanzisha karakana yako binafsi
Kupata zabuni za ujenzi
Ajira kwenye viwanda vya fanicha
Kozi ya Uashi (Masonry and Bricklaying)
Sekta ya ujenzi inahitaji mafundi uashi wenye ujuzi wa kutosha. Hii kozi hufundisha mbinu bora za ujenzi wa kuta, kuezeka, kutengeneza msingi, na usalama wa kazi za ujenzi.
Manufaa:
Ajira za moja kwa moja katika miradi ya ujenzi
Kuweza kujiajiri kwa kufanya kazi kwa watu binafsi
Mafunzo ya vitendo kwa zaidi ya 70%
Kozi ya Ushonaji na Ususi (Tailoring and Hairdressing)
Kozi hii ni maarufu sana hasa kwa vijana wa kike, lakini hata wavulana wanaweza kujiunga. Mafunzo yanahusisha ushonaji wa nguo, design za kisasa, ususi wa nywele, facial na make-up.
Nini kinachovutia:
Kujiingizia kipato ndani ya muda mfupi baada ya kuhitimu
Uwezo wa kufanya kazi popote – nyumbani, saluni au maonyesho
Soko la uhakika hasa kwenye sherehe na harusi
Kozi ya TEHAMA (ICT – Information and Communication Technology)
Katika ulimwengu wa kidigitali, kozi hii imekuwa na umuhimu mkubwa. Wanafunzi hufundishwa matumizi ya kompyuta, programu za ofisi, programu za biashara, mitandao na usalama wa data.
Faida kuu:
Ajira serikalini na sekta binafsi
Kuanzisha biashara ya huduma za IT
Kuweza kufanya kazi mtandaoni (freelancing)
Kozi ya Mapishi na Huduma ya Chakula (Food Production and Catering)
Sekta ya utalii na hoteli inahitaji wataalamu wa chakula kila siku. Kozi hii hufundisha mapishi ya kitaalamu, usafi wa chakula, huduma kwa wateja, na usimamizi wa migahawa.
Fursa baada ya mafunzo:
Ajira kwenye hoteli na migahawa mikubwa
Kuanzisha biashara ya chakula (catering services)
Kushiriki katika mashindano ya upishi kitaifa na kimataifa
Kozi ya Ufundi wa Simu za Mkononi (Mobile Phone Repair)
Simu ni sehemu ya maisha ya kila siku. Mafundi wa simu wanahitajika kwa wingi kutokana na ongezeko la matumizi ya simu. VETA hutoa kozi hii inayofundisha matengenezo ya simu, kubadili software, fixing hardware na calibration.
Nini kipya kwenye kozi hii:
Mafunzo ya vitendo kwa simu aina mbalimbali
Kujiunga na biashara ya matengenezo au kuuza vifaa
Mafunzo ya biashara kwa wale wanaotaka kufungua maduka yao
Kozi ya Uendeshaji Mitambo Mizito (Heavy Machinery Operation)
Kwa wale wanaotaka ajira kwenye miradi mikubwa ya serikali au taasisi binafsi, hii kozi ni bora. Inajumuisha kuendesha mitambo kama excavators, bulldozers, cranes, na forklifts.
Sababu za kuchukua kozi hii:
Ajira katika miradi ya ujenzi, migodi na bandari
Malipo mazuri kwa madereva wenye vyeti halali
Mafunzo salama na ya kitaalamu
Kozi ya Uendeshaji wa Basi na Gari Kubwa (Commercial Driving)
Kozi hii inawapa wanafunzi ujuzi wa kuendesha mabasi, malori, na magari ya mizigo pamoja na uelewa wa sheria za barabarani na usalama.
Manufaa:
Ajira kwenye kampuni za usafirishaji
Kujiunga na kazi za kimataifa
Mafunzo ya udereva wa kisasa pamoja na leseni
Soma Pia;
1. Kozi Nzuri za Kusoma Ngazi ya Diploma
2. Kozi Nzuri za Kusoma Ngazi ya Certificate
3. Vyuo vinavyotoa Kozi ya Food Science and Technology Tanzania