Katika juhudi za kukuza ujuzi wa kazi na kuongeza ajira nchini Tanzania, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inatoa kozi mbalimbali zinazolenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa vitendo katika nyanja tofauti za ufundi stadi. Kozi hizi zimegawanyika katika makundi mawili makuu: kozi za muda mrefu na kozi za muda mfupi.
Kozi za Muda Mrefu
Kozi hizi huchukua kati ya miezi sita hadi mitatu, kulingana na fani husika. Ada za mafunzo kwa kozi za muda mrefu katika vyuo vinavyomilikiwa na VETA ni shilingi 60,000/= kwa mwanafunzi wa kutwa na shilingi 120,000/= kwa mwanafunzi wa bweni. Mahitaji mengine yanakadiriwa kuwa kati ya shilingi 200,000 na 250,000, kulingana na fani na chuo husika.
Mfano wa Kozi za Muda Mrefu Zinazotolewa na VETA
Ufundi wa Magari (Motor Vehicle Mechanics)
Muda: Miezi 6
Ada: Shilingi 355,000
Chuo: VETA Chato
Umeme wa Majumbani (Electrical Installation)
Muda: Miezi 6
Ada: Shilingi 355,000
Chuo: VETA Chato
Ushonaji (Designing Sewing and Cloth Technology)
Muda: Miezi 5
Ada: Shilingi 355,000
Chuo: VETA Chato
Matumizi ya Kompyuta (Computer Application)
Muda: Miezi 3
Ada: Shilingi 165,000
Chuo: VETA Chato
Ufundi Bomba (Plumbing and Pipe Fitting)
Muda: Miezi 6
Ada: Shilingi 355,000
Chuo: VETA Chato
Kozi za Muda Mfupi
Kozi hizi huchukua kati ya wiki moja hadi miezi mitatu na hulenga kutoa ujuzi maalum kwa muda mfupi. Gharama za kozi hizi zinaanzia shilingi 50,000 hadi 320,000, kulingana na aina ya kozi na chuo husika.
Mfano wa Kozi za Muda Mfupi Zinazotolewa na VETA
Udereva wa Awali (Basic Driving Course)
Muda: Wiki 5
Ada: Shilingi 200,000
Chuo: VETA Mbeya
Udereva wa Magari ya Abiria (Passenger Service Vehicle – PSV)
Muda: Wiki 2
Ada: Shilingi 200,000
Chuo: VETA Mbeya
Udereva wa Pikipiki na Bajaji (Basic Motor Cycle Driving)
Muda: Wiki 2
Ada: Shilingi 70,000
Chuo: VETA Mbeya
Uhazili (Computer and Secretarial Course)
Muda: Miezi 3
Ada: Shilingi 200,000
Chuo: VETA Mbeya
Tecknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
Muda: Miezi 5
Ada: Shilingi 600,000
Chuo: VETA Mbeya
Utaratibu wa Kujiunga na Kozi za VETA
Ili kujiunga na kozi yoyote ya VETA, unapaswa kufuata hatua zifuatazo:
Kupata Fomu za Maombi: Fomu za maombi zinapatikana katika vyuo vya VETA au kupitia tovuti rasmi ya VETA.
Kujaza Fomu ya Maombi: Jaza fomu kwa usahihi kwa kutoa taarifa zote zinazohitajika.
Kuambatanisha Nyaraka Muhimu: Ambatanisha nakala za vyeti vyako vya elimu, cheti cha kuzaliwa, na picha za pasipoti.
Kuwasilisha Maombi: Wasilisha fomu ya maombi pamoja na nyaraka zote katika chuo cha VETA unachotaka kujiunga nacho.
Kufanya Mtihani wa Kujiunga:
Soma Pia;
2.Mfano wa Barua ya Kujiunga na JKT