Kikosi cha Yanga vs Wiliete Sc Leo 19/09/2025

Klabu ya Young Africans SC (Yanga SC) imewasili nchini Angola kwa ajili ya mchezo muhimu wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26. Timu hiyo inatarajiwa kushuka dimbani leo Ijumaa, Septemba 19, 2025 kwenye Uwanja wa Estadio 11 de Novembro, kumenyana na wenyeji Wiliete Sports Clube (Wiliete SC).

Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Huu ni mchezo wa muhimu sana kwa Yanga SC katika harakati zao za kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ambayo huwakutanisha na vilabu vikubwa kutoka barani kote.

Kwa mashabiki wa Yanga, hii ni fursa adhimu kushuhudia kikosi chao kikipambana kimataifa, wakilenga kupata matokeo mazuri ugenini ambayo yatakuwa chachu ya kujiweka kwenye nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Wiliete Sports Clube inaendelea kuwa moja ya wapinzani wenye historia thabiti kwenye ligi ya Angola, jambo linalotarajiwa kuongeza ushindani mkali kwenye mchezo huu. Ili kupata matokeo mazuri, Yanga SC italazimika kuonesha nidhamu ya hali ya juu, ustahimilivu wa kimataifa, na kutumia uzoefu wa wachezaji wao nyota ipasavyo.

Kikosi cha Yanga vs Wiliete Sc Leo 19/09/2025

error: Content is protected !!