Kwa AJIRA Mpya Kila Siku (BOFYA HAPA)
_____________________________________Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi amepokea kibali cha ajira mpya katika mwaka wa fedha 2024/2025 chenye Kumb.Na FA.97/228/01/A/2 cha tarehe 21/04/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora. Hivyo, Watanzania wenye sifa wanakaribishwa kutuma maombi ya nafasi za kazi zilizoanishwa katika Tangazo hili.
NAFASI 10 za Kazi Bariadi District Council August 2025
MASHARTI YA UJUMLA.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika utumishi wa Umma;
iii. Waombaji wote waambatishe malezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua
pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referres) watatu wa kuaminika;
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Certificates, – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma.
vi. “Testimonial”, “Provisional Results”, “Statement of Results”, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA NA NACTE).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 wa Mwaka 2010.
x. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika
xi. Mwisho wa kupokea maombi itakuwa tarehe 13/08/2025.