Kwa AJIRA Mpya Kila Siku (BOFYA HAPA)
_____________________________________Maboresho Kwenye Mfumo wa Ajira Portal
Job Overview
Maboresho Kwenye Mfumo wa Ajira Portal
UJAZAJI WA TAARIFA ZA ELIMU YA SEKONDARI
Kufuatia maboresho yaliyofanyika katika mfumo wa Ajira Portal, waombaji kazi
ambao tayari walikwishaweka taarifa zao kwenye mfumo wa Ajira Portal, wanapaswa kuhuisha taarifa zao za elimu ya Sekondari kwa kutumia namba ya mtihani wa kidato cha nne (Index Number) katika sehemu ya “Academic Qualifications”.
Kwa wale waliopita kidato cha sita, watatakiwa kuingiza namba ya mtihani wa kidato cha sita pia kwenye akaunti zao za mfumo wa Ajira Portal kwenye eneo la taarifa za kidato cha sita.
Mabadiliko haya ni ya lazima kwani waombaji kazi hawataweza kuendelea na uwasilishaji wa maombi ya kazi hadi pale taarifa zao za kielimu za kidato cha nne na sita ziwe zimeboreshwa.
Aidha, kufuatia maboresho haya, waombaji kazi hawatalazimika kuingiza nakala za vyeti vyao vya kidato cha nne na sita kwenye mfumo wa Ajira Portal, badala yake watatumia index number zao za kidato cha nne na sita PEKEE.
Kwa kufanya hivyo, taarifa zao zitachukuliwa moja kwa moja kutoka katika mfumo unaosimamiwa na BARAZA LA MITIHANI TANZANIA.
Kwa waombaji waliosoma kidato cha nne na sita nje ya nchi, watahusika pia na mabadiliko haya na watatumia ‘equivalence number’ wanazopokea kutoka BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA kuboresha taarifa zao.
2.UJAZAJI WA TAARIFA ZA KOZI WAOMBAJI WAMESOMEA
Eneo hili limefanyiwa maboresho pia kufuatia maoni ya wadau, awali eneo hili mtumiaji alitakiwa kuchagua kwanza ‘category’ ikifuatiwa na kozi yake, kwa sasa mtumiaji atatakiwa kutafuta (Search) moja kwa moja kozi yake bila kujali ipo kwenye ‘category’
gani na kisha kuichagua kozi yake.
3.MUONEKANO MPYA WA MFUMO WA AJIRA PORTAL
Mabadiliko ya teknolojia yameboresha pia muonekano wa mfumo na kuweka mazingira rafiki hasa kwa wale wanaotumia simu za kiganjani (Smartphone).
NB: Maboresho haya ni Katika Mfumo wa Ajira Portal Pekee na Pale Wasailiwa Wakiitwa Kwenye Usaili Watapaswa Kufika na Vyeti Vyao Halisi Kuanzia Kidato Cha Nne na Kuendelea.