Kuitwa Kazini Serikalini, UTUMISHI Call For Work July 2025

Kwa AJIRA Mpya Kila Siku (BOFYA HAPA)

_____________________________________

Angalia Majina ya Walioitwa Kazini Kupitia UTUMISHI – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) 2025

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali chenye hadhi ya Idara Huru kilichoanzishwa mahsusi kurahisisha mchakato wa ajira kwa watumishi wa umma. Sekretarieti hii ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1).

Majukumu Makuu ya PSRS ni kusaidia mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma. Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu cha 29(1), majukumu ya PSRS ni pamoja na:

  • Kusaka wataalamu mbalimbali wenye ujuzi maalum na kuandaa hifadhidata ya wataalamu hao kwa ajili ya urahisi wa ajira;
  • Kusajili wahitimu na wataalamu kwa madhumuni ya kumbukumbu na kujaza nafasi wazi;
  • Kutangaza nafasi wazi zinazojitokeza katika utumishi wa umma;
  • Kuwahusisha wataalamu husika kwa ajili ya kufanya usaili;
  • Kushauri waajiri juu ya masuala mbalimbali yahusuyo ajira; na
  • Kufanya jambo lolote au shughuli yoyote itakayopangiwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma.

Chombo hiki kinawaalika watu waliochaguliwa kujiunga na taasisi mbalimbali kwa ajili ya ajira.

Share this job

Search Job

error: Content is protected !!