Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kupitia Mitandao Ya Simu, Habari ya wakati huu mwanahabarika24, karibu katika makala hii fupi itakayoenda kukupa mwongozo juu ya jinsi ya kuweka pesa kwenye kadi ya mwendokasi kupitia mitandao ya simu.
Fahamu Kuhusu Wakala Wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)
Wakala Wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake. Jukumu kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo katika mkoa wa Dar es Salaam.
DART imeamua kurahisisha shuguli ya kufanya malipo kwa abiria wanaotumia usafiri wa mabasi ya mwendokasi kwa kupunguza foreni ya kukata tiketi kwa kuanzisha kadi janja ambayo itakua ikitumika katika kufanya malipo ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi.
Kuhusu Kadi ya Mabasi ya mwendokasi
Kadi ya mwendokasi ni kadi inayotumika kufanya malipo ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi pale abiria anapotaka kusafiri kwa kutumia mabasi hayo. kama unahitaji maelezo zaidi kuhusu kadi ya mwendokazi kama vile upatikanaji wake na jinsi inavyofanya kati tafadhari bonyeza HAPA.

Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kupitia Mitandao Ya Simu
Kama wewe ni mtumiaji wa usafiri wa mabasi ya mwendokasi kwenye safari zako jijini Dar es Salaam na unatumia kadi janja ya malipo ya nauli ya mwendokasi basi huna budi kufahamu jinsi ya kuweka salio/kuongeza pesa kwenye kadi yako kupitia mitandao ya simu kama vile Tigo, Vodacom, Airtel, Halotel na TTCL.
Njia za Kuweka Pesa Kwenye Kadi Ya Mwendokasi
Kunanjia kuu 3 ambazo mtumiaji wa kadi ya malipo ya mwendokasi anaweza kutumia katika kuweka au kuongeza pesa katika kadi yake mara baada linapoisha.
- Kungeza pesa kwa kutumia mitandao ya simu
- Kuongeza pesa kupitia benki
- Kuongeza pesa kupitia vituo vya mwendokasi
Hapa katika makala hii tutaangalia jinsi ya kuweka pesa kwa kutumia mitandao ya simu
1. Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kwa Vodacom
Ili uweze kuweka pesa kwenye kadi yako ya mwendokasi kupitia mtandao wa simu wa vodacom hasa M-Pesa tafadhari hakikisha umefuata hatua hizo hapo chini
- Piga *150*00#
- Chagua 4 Lipa kwa M-Pesa
- Chagua 5 Malipo ya Serikali
- Chagua 1 weka namba ya kumbukumbu
- Weka namba ya malipo
- Weka kiasi
- Weka namba ya Siri kukamilisha malipo
- Bonyeza 1 kufanya malipo ya AFCS
- Utapokea ujumbe kukujulisha ombi lako linashughulikiwa.
2. Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kwa Halotel
Ili kuweza kuongeza salio/pesa katika kadi yako ya mwendokasi baada ya salio kuisha kupitia mtandao wa simu wa Halotel (HaloPesa) unatakiwa kufuata hatua hizi hapa chini;
- Ingia kwenye ,menu ya HaloPesa kwa kupiga Piga *150*88#
- Kisha Chagua 4 – Lipa bili
- Kisha Chagua 5 – Malipo ya Serikali
- Ingiza kumbukumbu namba (Namab ya kadi ya Mwendokasi)
- Ingiza Kiasi unachotaka kukiweka kwenye kadi yako
- Ingiza Pin ya HaloPesa
- Bonyeza 1 ili kuthibitisha
- Utapokea ujumbe utakaokujulisha malipo ya muamala yanafanyiwa kazi.
3. Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kupitia Mtandao wa Tigo
Ili kuweza kuongeza salio/pesa kwenye kadi yako ya mwendokasi kupitia mtandao wa simu wa Tigi tafadhari fuata maelekezo hapa chini
- Piga *150*01#
- Chagua 4 Lipa Bili
- Chagua 5 Malipo ya Serikali
- Chagua 1 ingiza namba ya malipo
- Weka kiasi
- Chagua 2 ingiza kiasi
- Weka namba ya siri kuthibitisha
- Utapokea ujumbe unaokujulisha malipo yamekamilika
4. Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kupitia Airtel
Hapa chini ni maelekezo ya njinsi mtumiaji wa mtandao wa simu wa Airtel anavyoweza kuongeza pesa/salio katika kadi yake ya mwendokasi. Tfadhari kwa wewe unaetumia Airtel fuata hatua hizi hapa chini
- Piga*150*60#
- Chagua 5 Lipa Bill
- Chagua 5 Malipo ya Serikali
- Chagua 1 Ingiza control number
- Ingiza kiasi cha pesa
- Weka namba ya Siri kulipia
- Utapokea ujumbe utakaokujulisha ombi lako linashughulikiwa.
5. Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi Kupitia Ttcl
Kwa wewe mtumiaji wa mtandao wa simu wa Ttcl basi unaweza kufuata hatua hizi hapa chini ili kuweza kuweka/kuongeza pesa kwenye kadi yako ya mwendokasi
- Piga *150*71#
- Chagua 4 Lipa bili
- Chagua 6 Malipo ya Serikali
- Weka namba ya kumbukumbu
- Weka kiasi
- Ingiza namba ya siri kuthibitisha malipo
- Utapokea ujumbe unaokujulisha malipo yamepokelewa
Kama tulivyosema hapo awali hapo juu ni jinsi wewe mtumiaajiwa mtandao wa simu wa Vocadom, Tigo, Ttcl, Halotel na Airtel unavyoweza kutumia mitandao hoyo ya simu kuweza kuongeza/kuweka pesa kwenye kadi yako ya Mwendokasi.
Kumbuka kadi hii ya malipo ya usafiri wa mwendokasi ni maalumu kwa malipo ya mwendokasi tu na hutumika kwenye mashine maalunu za kulipia zilizopo vituni, kadi hii haiwezi kutumika katika kufanya malipo mengine ya aina yoyote ile.
Mawasiliano na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
Adress
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
Ubungo Maji, Morogoro Road,
S. L. P 724, 16103
Dar es salaam, Tanzania.
Email; [email protected]
Simu; 0800 110 147, +255-22-27000486/280
Hitimisho
Kuhakikisha kadi yako inapesa za kutosha katika matumizi ya kiusafiri kwenye usafiri wa mabasi yaendayo mwendo wa kasi ni muhimu zaidi. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kujua njia mbali mbali unazoweza kuzitumia ili kuweza kuongeza salio katika kadi yako ya Mwendokasi, ukiachilia mbali njia ya kutumia mitandao ya simu lakini pia unaweza kuweka salio katika kadi yako ya mwendokasi kwa kutumia njia ya benki na kwa kutembelea maafisa wa mwendokasi walipo katika vituo vya mabasi ya mwendokasi.