Jinsi Ya Kurudisha Channel Zilizopotea Kwenye Kisimbizi Cha Azam TV, Jinsi ya kutafuta signal azam TV, Habari mwanafamilia wa Azam Tv, karibu katika makala hii fupi itakayoweza kukupa mwongo wa namna gani unavyoweza kurejesha channel zilizopotea kwenye king’amuzi chako cha Azam Tv.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Je umekumbwa na changamoto ya kupotea kwa channel kwenye decoder yako ya Azam Tv? Basi usijali kwani makala hii inamwongozo wa wewe kufuata ili kuweza kurudisha channel amabzo zimepotea kwenye kingamuizi chako cha Azam Tv.
Jinsi Ya Kurudisha Channel Zilizopotea Kwenye Kisimbiz Cha Azam TV
Azam Tv ni moja kati ya kampuni maarufu zaidi nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla wake hii ni nkutokana na uwepo wa channel bora zaidi katika visimbuzi vyake.
Makala hii inalenga kukupa mwongozo wewe mtumiaji wa kisimbuzi cha Azam Tv kama umekumbwa na changamoto ya kupotea kwa channel za Azm Tv.
Sababu zinazoweza Pelekea Kupotea Kwa Channel kwenye Kisimbuzi Cha Azam Tv
Kunasabu mbalimbali amabao kwa kiasi zinaweza kusababisha kisimbuzi chako cha Azam Tv kuweza kupoteza Channel zake. Hapa Ni baadhi ya sababu tu zinazoweza kupelekea changamoto hiyo.
- Tatizokutoka kwenye Atena au LNB
- Uingizaji mpya wa setingi (Configuration)
- Mbadiliko ya masafa ya channel
Jinsi Ya Kurudisha Channel Zilizopotea Kwenye Decoder ya Azam TV
Baada ya kufahamu ni sababu gani zinaweza kupelekea kupotea kwa channele kwenye kisimbuzi cha Azam Tv sasa embu tutazame ni hatua gani unaweza kuzifanya ili kuweza kurudisha channel hizo kwenye kisimbuzi chako cha Azam Tv.
Kuna hatua kadhaa wewe mtumiaji wa kisimbuzio cha Azam Tv uliokutwa na changamoto ya kisimbuzi chako kupoteza channel zake, hapa chini ni miongoni mwa hatua hizo.
1. Tafuta Upya Channel (Rescan)
Kama channel hazionekani kwenye kismbuzi chako cha Azam Tv unaweza kutumia setting ya ya kutafuta upya channel. Njia hii itatafuta upya na kuweka mpangilio mpya wa channel kama kunachannel zilipotea kutokana na mabadiliko ya masafa basi zitarejea kwa masafa mapya.
Njinsi ya Kutafuta Upya Channel kwenye Azam Tv
- Nenda kwneye serring ya kisimbuzi chako kupitia rimoti
- Kisha bonyeza palipoandikwa search/Tafuata
- Kisha nenda palipo andikwa Outo
- Subiri kwa muda na channel zako zote kulingana na kifurushi chako zitarudi.
2. Angali Muunganiko wa Atena/Dishi na Kisimbuzi cha Azam Tv
– Kama njia ya kutafuta haikuzaa matunda basi itakupasha uweze kutizama kwa umakini muunganiko uliopo kati ya Atena au Dishi na kisimbuzi chako cha Azam Tv kama kimeunganishwa vizuri, kagua waya unaotoa mawasiliano kutoka kwenye Atena au Dishi hadi kwenye Kisimbizi chako kama uko vizuri.
– Pia hakikisha kua Atena au Dishi lako liko kwenye mwelekeo sahihi wa mawinbi ya picha ya Azam Tv, kama huna uhakika wa uwelekeo wa Arena au Dishi lako tafadhari unaweza kumuita mtaala akurekebishie.
3. Tazama Muunganiko wa Kisimbuzi Chako na TV Yako
Kama njia ya 1 na 2 ziko sawa na bado unakumbwa na taizo la kutokuwepo kwa picha/ channel kwenye kisimbuzi chako basi ianawezeekana pia muunganiko wa dekoda yako na Runiga (TV) yako hauko sahihi jaribu kutazma na kujihakikishia kua kebo zote zimechomekwa mahara sahihi na hazina shida yoyote ile.
4. Tazama Kiwango cha Signal wakati wa Utafutaji Channel
Wakati unafanya zoezi la kutafuta channel upya jaribu kuangalia kiwango cha Signal Strength na Signal Quality. Kiwango cha kawaida kinachopendekezwa wakati wa utafutaji ni 60%. Kama utagundua ya kua kiwango cha signal kipo cjhini ya asilimia 60 basi jalibu kugeuza uwelekeo wa Atena au Dishi hadi signal itakapo panda na kufika 60% na kuendelea hii inasaidia utafutaji channel kuwa mwepesi zaidi.
5. Fanya Factory Reset
Hii ni hatua ya mwisho kabisa baada ya hatua zote hapo juu kushikana. Ikiwa umefanya hatua zote hapo juu na bado channel hazijarudi basi hauna budi kufanya factory reset. Njia hii hufuta data na mipangilio yote ya awali na kuanza kuweka upya. Baada ya kufanya factory reset itakupasa uweze kuweka stting zote upya.
Njinsi ya Kufanya Factory Reset kwenye Dekoda ya Azam Tv
Fuata hatua hizi hapa chini nili kuweza kufanya factory reset ya kisimbuzi chako cha Azam Tv
- Chukua rimoti yako na uende sehemu ya setting
- Chagua factory reset
- Kisha bonyeza ok
- Subili kwa dk na stting zote za awali zitaondoka
- Anza kuingiza setting upya
- Furahia channel zako.
Wasiliana na Azam Huduma kwa Wateja
Kama bado changamoto inaendelea unawaza kuwasiliana na watu wa Azam huduma kwa awate, kwa kufanya hivyo unaweza kupata msaada wa kiufundi kutoka kwao.
Njisi ya kuwasiliana na Azam Tv Huduma kwa Wateja
Kunanjia kuu mbili za kuwasiliana na watu wa Azam Tv huduma kwa wateja amabzo ni
- Unaweza tembelea moja kwa moja ofisi za Azam Tv zilizopo Tazara jijini Dar es Salaam mkabara na daraja la juu la Mfugale
- Unaweza kwasiliana nao kwa kupiga simua – 0764 700 222 na 0784 108 000 au kwa email [email protected]
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Njinsi ya Kuweza Kutazama Channel za Azam Tv Bure
2. Orodha ya Channel Zote za Visimbuzi Vya Azam TV
3. Orodha ya App Nzuri za Kuangalia Mpira Live Kwenye Simu