Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS ni rahisi na haraka. Njia hii ni mbadala wa njia ya zamani ya USSD ambayo ilitumika awali. Kupitia huduma hii mpya, mtu anaweza kupata namba yake ya NIDA kirahisi zaidi.
Hatua za Kufuata lli Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS
1. Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
- Hakikisha una salio la kutosha kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS).
2. Andika ujumbe mfupi wenye jina lako kamili
- Andika jina laoko kamili kama ulivyojiandikisha wakati wa kujisajili, Mfano “Alex John Msekwa”
3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15096.
- Baada ya kuandika ujumbe wako itakubidi kuituma ujumbe huo kwenda kwenye namba 15096
4. Subiri ujumbe wa jibu kutoka NIDA.
- Baada ya kutuma ujumbe wako tafadhari subiri ndani ya muda mfupi utapokea ujumbe kutoka NIDA wenye namba yako ya NIDA
Kumbuka huduma hii ya kutazama namba yako ya NIDA kwa njia ya SMS ni njia ya bure kabisa haina gharama yoyote ile na inapatikana katika mitangao yote ya simu.
Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia USSD
USSD kwa kirefu (Unstructured Supplementary Service Data)hii ni njia ya kuangalia namba yako ya NIDA kwa kutumia code maatumu za simu. Hii pia ni njia rahisi kwenye kupata namba yako ya NIDA
Hatu za Kupata Namba ya NIDA Kwa USSD
- Piga *152*00# kwenye simu yako ya mkononi.
- Chagua namba 3 (Ajira na Utambuzi).
- Chagua namba 2 (NIDA).
- Ingiza majina yako kamili kama ulivyo jisajili na NIDA mfano, “Alex John Msekwa”
- Kisha ingiza namba ya simu uliyojaza kwenye fomu ya maombi
- Kubali ombi lako.
- Utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye namba yako ya NIDA.
Umuhimu wa Kua na Namba ya NIDA
Namba ya NIDA ni zaidi ya namba tu. Ni kitambulisho chako cha kipekee kinachokuunganisha na huduma mbalimbali za serikali na zisizo za serikali. Hapa kuna baadhi ya sababu kwa nini unahitaji kujua namba yako ya NIDA:
- Huduma za Serikali: Namba ya NIDA inahitajika kwa huduma nyingi za serikali, kama vile kusajili laini za simu, kupata hati ya kusafiria, na kupiga kura.
- Huduma za Kifedha: Benki na taasisi nyingine za fedha zinahitaji namba ya NIDA ili kufungua akaunti na kutoa mikopo.
- Ajira: Waajiri wengi huomba namba ya NIDA ili kuthibitisha utambulisho wa waombaji kazi.
- Usalama: Namba ya NIDA husaidia katika kuimarisha usalama wa taifa kwa kuzuia uhalifu na vitendo vingine viovu.
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Namna Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (NSSF Balance Check)
2. Namna ya Kujiunga na Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI
3. Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari 2024 (TMS Traffic Check)
4. Namna ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa unamaswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku