Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima 2025
Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima, Cheti cha kuzaliwa ni utambulisho au hati yenye umuhimu mkubwa sana kwa raia wa taifa lolote lile iwe Tanzania au nje ya mipaka ya Tanzania. Cheti cha kuzaliwa ni hati inayobeba taarifa za msingi juu ya mtu kuhusu uzaliwa wake, kama vile mahari alipozaliwa, majina ya baba na mama, tarehe ya kuzaliwa na jina la muhusika. Cheti hiki hutumika katuka utambulisho wa mmiliki kwenye maeneo mbali mbali, kama vile mashuleni pia hata kwenye kuomba ajira, lakini pia katika taasisi a kibenki cheti cha kuzaliwa hutumika kuthibitisha taarifa za mfunguaji akaunti au mtumiaji akaunti.
Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima & Mtoto Chini Ya miaka 10
Pamoja na sababu tulizo zitaja hapo juu kuhusu umuhimu wa cheti cha kuzaliwa imekua tatizo kwa baadhi ya watu kuto kua nav yeti hivyo vya kuzaliwa nah ii inaweza kusababishwa na mambo kadha wa kadha, mfano ni kutokua wa ufahamu wa kutosha kwa wazazi juu ya umuhimu wa cheti hicho kwa mtoto wao aliki pia mazingira yaupatikanaji wa cheti hicho au pia hata migogoro miongoni mwa wazazi inawaza pelekea mtoto kuto patiwa cheti chake cha kuzaliwa japo wapo wazazi ambao mara baada ya kupata mtoto hufuatilia hatua kwa hatua juu ya cheti hiki cha kuzaliwa.
Ikumbukwe kua umiliki wa cheti cha kuzaliwa pia unaweza kukufungulia mlango wa kushiliki katika mambo mbalimbali na kama hutokuanacho pia inaweza kuwa changamoto kwako kwenye kupata baadhi ya huduma hivyo ni vyema kuhakikisha unacheti cha kuazliwa. Mfano kwa sasa huwezi jiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA bila ya kua ana cheti cha kuzaliwa.
Hivyo basi sisi kama Habarika24 tumeamua kuandika Makala hii ili kutoa mwongo wa jinsi gani wewe ambaye hukuweza kupata cheti cha kuzaliwa ulipokua mdogo unaweza kufanya ili kukipata, kumbuka mwongo huu umejikita kwa raia wa Tanzania tu, hapa tutaenda kukuelekeza kuhusu taratibu zote za kufuata ili kupata cheti cha kuzaliwa ikiwemo iina za vyeti vya kuzalia njia za kuomba cheti cha kuzaliwa na vitu vya msingi vya kua navyo katika mchakato mzima wa kuomba cheti cha kuzaliwa.
Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima na Mtoto
Ili kupata cheti cha kuzaliwa kuna utaratibu maalumu wa kufuata ila utarati huo hutofautiana kulingana ma muda au kipindi kipi unachotaka kuomba cheti cha kuzaliwa, hivyo basi hapa utapata maelezo yote na taratibu zote za kuomba cheti cha kuzaliwa kuanzi mtoto mdogo aliyezaliwa hati hatua ya mtu mzima
Kupata Cheti Cha Kuzaliwa kwa Mtoto Aliezaliwa Ndani ya Siku 90
Kwa mtoto aliyezaliwa ndani ya siku 90 utarati wake wa upataji wa cheti cha kuzaliwa ni rahisi mmno na wa haraka zaidi hasa kama wazazi wana taarifa kamili za kuzaliwa kwa mtoto wao.
Hapa chini tumeweka utaratibu wote amabo utaweza kuufuata pale unapotaka kuomba cheti cha kuzaliwa kwa mtoto aliyezaliwa ndani ya siku 90;
– Tangazo la Kizazi, Pindi mtoto atakapozaliwa mzazi au mlezi hakikisha unapata tangazo la kizazi kabla haujaomdoka kutoka hospitali tangazo hilo hutolewa na mtoa huduma hapo hapo kituo cha afya.
– Kizazi Nyumbani, Kama mtoto wako alizaliwa nyumbani basi wewe mzazi au mlezi hakikisha umetoa taarifa za kuzaliwa kwa mtoto kwa afisa mtendaji wa Kijiji alipo zaliwa mtoto au kwa msajili wa vizazi na vifo ndani ya wilaya husika ndani ya siku zisizopungua 90 ili kuasidi kupata Tangazo la kizazi.
– Wasilisha Tangazo la Kizazi, Mara baada ya kupata Tangazo la kizazi basi mzazi au mlezi utapaswa kuipeleka hati hiyo kwa msajiri wa Vizazi na Vifowa wilaya alipo zaliwa mtoto.
Lipa Ada Ya Usajili, Mara baada ya kuwasilisha hati ya Tangazo la kizazi utatakiwa kulipia ada ya usajili amabayo ni kiasi cha shilingi 8,000/=, Mara baada ya kukamilisha malipo utasubiri na cheti chako kitatoka.

Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima & Mtoto Chini Ya miaka 10
Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtoto mwenye Siku 90 Lakini Chini ya Miaka 10
Utaratibu huu unahusisha hatua zaidi ikilinganishwa na usajili wa ndani ya siku 90.
Fomu ya Maombi: Mzazi au mlezi anatakiwa kujaza na kuwasilisha Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3. Fomu hii inapatikana katika ofisi za Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA) au ofisi za serikali za mitaa.
Picha: Mzazi au mlezi anatakiwa kuambatanisha picha ya mtoto (passport size) kwenye fomu ya maombi.
Nyaraka za Ushahidi: Ili kuthibitisha taarifa za kuzaliwa, mzazi au mlezi anatakiwa kuambatanisha nyaraka kama vile:
- Pasipoti
- Cheti cha kumaliza elimu ya msingi au sekondari
- Kadi ya kliniki ya mtoto
- Cheti cha ubatizo (ikiwa inafaa)
- Barua kutoka ofisi za serikali (mfano, ofisi ya mtendaji wa kata/kijiji)
Ada ya Usajili: Baada ya kuwasilisha fomu na nyaraka, mzazi au mlezi atalipa ada ya usajili ambayo kwa sasa ni shilingi 8,000/=.
Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima Zaidi ya Miaka 10
Utaratibu huu unahitaji umakini zaidi na nyaraka za ziada kutokana na muda mrefu uliopita.
Fomu ya Maombi: Mzazi au mlezi hujaza na kuwasilisha Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3. “Bofya Hapa Kupakua Fomu”
Picha: Picha ya mtoto (passport size) inahitajika.
Nyaraka za Ushahidi: Mzazi au mlezi anatakiwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali kama vile:
- Kadi ya kliniki ya mtoto
- Cheti cha ubatizo (ikiwa kipo)
- Barua kutoka mamlaka za serikali (mfano, ofisi ya mtendaji wa kata/kijiji)
- Cheti cha kumaliza elimu ya msingi au sekondari
Nyaraka za Utambulisho (kwa waliozaliwa zamani): Kwa wale waliozaliwa miaka mingi iliyopita, wanatakiwa kuambatanisha nyaraka za ziada kama vile:
- Kadi ya Utaifa pamoja na Kadi ya Kura au Bima ya Afya.
- Leseni ya Gari (lazima iambatane na Kadi ya Utaifa au Kadi ya Kura).
Ada ya Usajili: Ada ya usajili kwa utaratibu huu ni shilingi 20,000/=
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20
2. Orodha ya Wanamziki Weneye Pesa Nyingi Zaidi Tanzania
3. Mfano Wa Makosa ya Jinai Pamoja na Vifungu Vyake
5. Jinsi ya Kujisajili SokaBet