Jinsi ya Kununua Vipande Vya Uwekezaji Vya UTT AMIS, Jinsi ya Kufanya Uwekezaji Kwenye Mfuko wa UTT AMIS, jinis ya kununua vipande kwenye mfuko wa uwekezaji wa UTT AMIS, Habari karibu kwenye kurasa hii amabayo itaenda kukupa mwongozo wa namna ya kuweza kufanya uwekezaji kwenye mfuko wa uwekezaji wa UTT AMIS
Jinsi ya Kununua Vipande Vya Uwekezaji Vya UTT AMIS
Baada ya kufungua akaunti yako kwenye mfumo wa UTT AMIS sasa unaweza kuanza kufanya uwekezaji wako kwa kununua vipande kulingana na mfuko uliojiunga. Kufanya uwekezaji kwenye mfumo wa UTT AMIS unaweza kutumia njia kuu 2 ambazo ni
- Uwekezaji wa UTT AMIS kwa kutumia mitandao ya Simu
- Uwekezaji wa UTT AMIS kwa njia ya huduma ya njia za kibenki
Fungua akaunti yako ya uwekezaji kupitia huduma ya SimImvest👆. Haijalishi una simu Janja au smartphone.
Kumbuka ; ukishapata akaunti yako, jaza form ya kujiunga ili kukamilisha usajil,
Kisha endelea kuwekeza kwa njia ya mitandao ya simu au huduma za kibenki ( CRDB, NMB, Stanbanc, NBC).
Ununuji wa Vipande Vya UTT AMIS kwa kutumia mitandao ya Simu
Kama unahitaji kufanya uwekezaji wako kwa kutumia njia ya mitandao ya simu basi unaweza kufuata hatua hizi hapa kwa kila mtandao wa simu
1. Kununua Vipande vya UTT AMIS Kupitia Mtandao wa M-Pesa
kwa kutumia mtandao wa vodacom (M-Pesa) fuata hatua zifuatazo
Ingia kwenye simu yako na upige *150*00#
1. Kisha chagua Lipa kwa M-Pesa
2. Chagua kwenye orodha
3. Kisha bonyeza ZAIDI
4. Kisha chagua “Michango ya Uananachama”
5. Kisha chagua “UTTAMIS”
6. Ingiza kumbukumbu namba( Hapa utajaza akaunti namba yako ya Mfuko)
7. Kisha weka kiasi
8. Weka namba yako ya siri ya M-Pesa
9. Kisha thibitisha malipo.
2. Kununua Vipande vya UTT AMIS Kupitia Mtandao wa Airtel Money
Ili kuweza kununua vipande vya UTT AMIS kupitia mtandao wa Airtel Moneytafadhari embu fuata hatua zifuatazo
Ingia kwenye simu yako na upige namba *150*60#
1.Kisha chagua namab 5, Lipa Bili
2. Kisha namba 4, Weka lipa namba( Hapa utaweka namba ya kampuni UTT AMIS)
3. Kisha namba 3, Weka kiasi cha pesa
4. Kisha namba 4, Ingiza akaunti ya mfuko wako wa UTT AMIS
5. Kisha namba 5, Kamilisha mwamala
6. Ingiza namaba ya siri ya Airtel Money
7. Thibitisha malipo.
3. Kununua Vipande vya UTT AMIS Kupitia Mtandao wa Tigo Pesa
Pia unaweza kununu vipande vya UTT AMIS kwa kutumia mtandao wa simu wa Tigo Pesa, kununua vipande vya UTT AMIS kupitia tigo pesa embu fuata hatua zifuatazao.
Ingia kwenye simu yako na upige namba *150*01#
1. Kisha uchague namba 4, Lipa Bili
2. Chagua namba 2, kupata majina ya Kampuni
3. Kisha chagua namba 9, UTTAMIS & ELIMU
4. Kisha chagua namaba 1, UTTAMIS
5. Kisha weka namba ya Kumbukumbu( Namba ya Akaunti yako ya UTTAMIS)
6. Ingiza kiasi cha pesa unachotaka kununulia vipande
7. Kisha weka neno siri la Tigo Pesa
8. Thibitisha malipo
Ununuji wa Vipande Vya UTT AMIS kwa kutumia Huduma za Kibenki
Njia nyingine amabyo mwekezaji wa jipande vya UTT AMIS anweza kutumia ili kununulia vipande hivyo ni kipitia njia ya huduma za mitandao ya kibenki.Mitandao ya kibenki inayofanya kazi na kampuni ya UTT AMIS ni pamoja na
- CRDB
- NMB
- Stanbanc
- NBC
Hapa chini tutaenda kukuonyesha hatua za kufuata kwa kila benki ili kununua vipande vya UTT AMIS.
1. Njinsi ya Kununua Vipande vya UTT AMIS Kupitia Benki ya CRDB
Ili uweze kununua vipande vya UTT AMIS kupitia benki ya CRDB basi unaweza kufuata hatua zifuatazo;
Chukua simu janja yako na uende play Store au App Store na upadownload Simbankig App
1. Kisha ingia kwenye akaunti yako ya Simbanking kupitia App
2.Nenda sehemu ya Malipo(Payment)
3. Kisha nenda malipo ya ziada
4. Kisha shuka chuini hadi utakapoona UTT AMIS na ubonyeze hapo
5.Ingiza namba ya Incoive
2. Njinsi ya Kununua Vipande vya UTT AMIS Kupitia Benki ya NMB
Pia unaweza kununua vipande vya UTT AMIS kupitia benki ya NMB ili kufanya hivyo tafadhari embua fuata hatua zifuatazo;
Nenda kwenye simu janja yako na upakue App ya NMB Mobilie App, iwe Play Store au App Store
1. Kisha ingia kwenye akaunit yako ya NMB
2. Nenda lipa Bili
3. Malipo ya Biashara
4. Ingiza namba ya biashara – 100020
5. Ingiza kumbukumbu (Namba ya akaunti yako ya UTT AMIS)
6. Hakiki namba ya malipo
7. Weka kiasi cha malipo unachohitaji kulipa
8. Thibitisha malipo
3.Njinsi ya Kununua Vipande vya UTT AMIS Kupitia Benki ya Stanbanc
Mfuko wa uwekezaji wa UTT AMIS pia unaruhusu ununuaji wa vipande kwa kutumia banki ya Stanbanc, Ili kutumia banki hii kuweza kufanya uwekezaji wako kwa kununua vipande vya mfuko uluiojiunga tafadhari embu fuata hatua zifuatazo.
Ili kuweza kununua vipende ya UTT AMIS kupitia Benki ya Sanbanic itakupasa kutembelea tawi lolote la Benki ya Stanbic lililopo kalibu nawe na kuweza kununua. Hakikisha unabeba namba ya akaunti yako ya UTT AMIS ili kufanya malipo sahihi kweye akaunti yako
Huduma ya kununua vipande vya Mfuko wa uwekezaji wa UTT AMIS kupitia benki ya Stanbic ni bure kwa watu wote.
Mapendekezo ya Mhariri;
Jinsi ya Kujiunga na Mfuko wa Uwekezaji Wa UTT AMIS
Mwongozo wa Bei ya Vipande vya UTT AMIS 2025