Jinsi ya Kununua Tiketi ya Treni za GSR Kupitia M-Pesa
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA TELEGRAM CHANNEL YETU
Jinsi ya Kununua Tiketi ya Treni za GSR Kupitia M-Pesa, Je, umewahi kujikuta ukitaka kusafiri kwa treni za GSR lakini huna muda wa kwenda kununua tiketi ofisini? Usijali! Teknolojia ya mtandao wa Vodacom imekuja na suluhisho la haraka na rahisi. Leo katika makala hii fupi tutaangalia jinsi unavyoweza kununua tiketi ya treni za GSR kupitia M-Pesa, mfumo wa malipo wa simu unaotumika sana nchini Tanzia.
Jinsi ya Kununua Tiketi ya Treni za GSR Kupitia M-Pesa
Hapa chini tutaenda kujadili juu ya njia tofdauti tofauti utakazoweza kuzitumia ili kununua tiketi yako ya safari ya treni ya GSR kwa kutumia mtandao wa Vodacom (M-Pesa)
Hatua za Kununua Tiketi
Kwa M-Pesa super app
1. Baada ya kupokea control number fungua app ya M-Pesa
2. chagua mini app ya GEPg
3. Kisha chagua malipo
4. Kisha weka control number kukamilisha malipo yako

Kwa ussd
1. Piga *150*00#
2. Chagua namba 4 malipo ya serikali
3. Kisha weka control number kukamilisha malipo
Mambo ya Kuzingatia
- Hakikisha una salio la kutosha kwenye akaunti yako ya M-Pesa kabla ya kuanza mchakato.
- Weka ujumbe wa uthibitisho kutoka GSR. Utahitajika kuonyesha huu wakati wa kupanda treni.
- Ikiwa utapata shida yoyote wakati wa kufanya malipo, unaweza kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja cha GSR au M-Pesa kwa msaada.
Hitimisho
Kununua tiketi ya treni za GSR kupitia M-Pesa ni njia rahisi, ya haraka na salama. Inakuwezesha kupanga safari yako kwa urahisi bila kuhitaji kutembelea ofisi za GSR. Jaribu leo na uone jinsi inavyoweza kuokoa muda wako wa thamani.
Mapendekezo ya Mhariri
Ratiba ya treni za SGR Dar es Salaam na Morogoro
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa una maswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi