Jinsi Ya Kukata Tiketi Ya Basi Mtandaoni, Kukata tiketi ya basi kwa njia ya Simu, Habari ya wakati huu ewe msafiri wa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kwa usafiri wa basi, karibu katika makala hii fupi ambayo itaenda kukupa mongozo wa jinsi ya kukata tiketi ya basi mtandaoni. Je unatarajia kusafiri kutumia usafiri wa basi, basi makala hii itakua na umuhimu mbwa sana kwako kwani utaweza kujua jinsi ya kuweza kukata tiketi yako kwa njia ya mtandao (Kukata tiketi ya basi kwa Simu).
Kumekua na maswali mengi yanayoulizwa na baadhi ya abiria juu ya kama inawezekana kwa msafiri kuweza kukata tiketi yake kwa njia ya mtandao (Online tiket), jibu ni ndio lakini ni kwa baadhi ya kampuni za mabasi zenye kutoa huduma za ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao.
Umuhimu wa Huduma Ya Kukata Tiketi Mtandaoni
Njia hii ya kukata tiketi kwa njia ya mtandao inafaida kubwa sana, miongoni mwa faidia za kukata tiketi kwa njia ya mtandao ni pamoja na;
- Kuepuka foleni ya ukataji wa tiketi
- Huchukua mda mfupi zaidi
- Usalama wa kifedha
- uchaguzi wa siti ya basi
- Kuepusha gharama
Jinsi Ya Kukata Tiketi Ya Basi Mtandaoni
Makampuni baadhi ya usafirishaji kwa njia ya basi wameweza kurahisisha mchakato wa ukataji wa tiketi za mabasi kwa kuanzisha mifumo ya mdandaoni ya ukataji wa tiketi. Hapa tutaenda kuangazia baadhi ya makampuni na jinsi unavyoweza kukata tiketi kupitia makampuni hayo
1. Abood Bus Service
Abood ni moja kati ya kampuni za mabasi kubwa na za muda mrefu kama wewe ni msafiri kwenye mkoa ambao basi za Abood zinafanya safari zake basi habari njema ni kua kwa kutumia simu au kifaa chako chenye uwezo wa kuindia mtandaoni unaweza kukata tiketi ya safari yako. Cha kufanya fuata hatua zifuatazao;
- Ingia kwenye tovuti rasimi ya kampuni ya Abood Bus Service kwa kutumia link hii hapa – https://aboodbus.co.tz/
- Kwenye ukrasa wa tovuti ya Abood jaza taarifa zako za safari kama vile, Unakotoka, Unako kwenda na siku ya safari
- Baada ya kujaza taarifa bonyeza neno “Search”
- Baada ya kubonyeza orodha ya mabasi itafunguka na taarifa zake kama muda wa safari na bei ya nauli
- Kisha bonyeza neno “Book Tiket”
- Ukrasa wa mpangilio wa siti utafunguka na utachagua siti uipendayo kulingana na maelekezo ya mfumo kisha utabonyeza “proceed”
- Mfumo wa tiketi utafunguka na utajaza taarifa kutokana na maelekezo na kisha mbonyeza “Endelea” ili kumaliza hatua na kukata tiketi yako.
2. Shabiby Line
kwa wasafiri wa kampuni ya Shabiby line, kampuni hii pia inamfumo wa ukataji tiketi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yao, cha kufanya fuata hatua zifuatazo hapa chini ili kukata tiketi ya basi ya Shabiby Line.
- Ingia kwenye tovuti rasimi ya kampuni ya Shabiby Line kwa kutumia link hii hapa – https://shabiby.co.tz
- Kwenye ukrasa wa tovuti ya Shabiby Line nenda kwenye upande wa NUNUA TIKETI na ujaze taarifa zako za safari kama vile, Unakotoka, Unako kwenda na siku ya safari
- Baada ya kujaza taarifa bonyeza neno “Angalia Ratiba”
- Baada ya kubonyeza orodha ya mabasi itafunguka na taarifa zake kama muda wa safari na bei ya nauli na daraja la basi
- Kisha bonyeza neno “Nnua Tiketi”
- Ukrasa wa mpangilio wa siti utafunguka na utachagua siti uipendayo kulingana na maelekezo ya mfumo kisha utabonyeza “Hifadhi Tiketi”
- Mfumo wa tiketi utafunguka na utajaza taarifa kutokana na maelekezo na kisha mbonyeza “Endelea” ili kumaliza hatua na kukata tiketi yako.
3. Happy Nation
Kampuni ya mabasi ya Happy Nation nayo ni miongoni mwa kampuni za usafirishaji zenye kutoa huduma ya ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao, ili kuweza kukata tiketi ya basi katika kampuni ya Happy Nation kwa njia ya mtandao tafadhari fuata hatua zifuatazo;
- Ingia kwenye tovuti rasimi ya kampuni ya Shabiby Line kwa kutumia link hii hapa – https://www.happynation.co.tz/
- Kwenye ukrasa wa tovuti ya Happy Nation jaza taarifa zako za safari kama vile, Unakotoka, Unako kwenda na siku ya safari
- Baada ya kujaza taarifa bonyeza neno “Tafuta Basi”
- Baada ya kubonyeza orodha ya mabasi itafunguka na taarifa zake kama muda wa safari na bei ya nauli na daraja la basi
- Kisha bonyeza neno “Nnua Tiketi”
- Ukrasa wa mpangilio wa siti utafunguka na utachagua siti uipendayo kulingana na maelekezo ya mfumo kisha utabonyeza “Hifadhi Tiketi”
- Mfumo wa tiketi utafunguka na utajaza taarifa kutokana na maelekezo na kisha mbonyeza “Endelea” ili kumaliza hatua na kukata tiketi yako.