Jinsi ya Kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania 2025
Ikiwa unavutiwa na kazi ya kulinda na kutumikia taifa lako, kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania ni hatua muhimu. Makala hii itakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kwa mwaka 2025, ikijumuisha sifa zinazohitajika, mchakato wa maombi, na vidokezo vya mafanikio.
Sifa za Kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania 2025
Ili kuwa miongoni mwa waliochaguliwa, unapaswa kutimiza vigezo vifuatavyo:
1. Uraia na Umri
-
Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
-
Kwa waombaji wa kidato cha nne, sita, na astashahada: Umri kati ya miaka 18 na 25.
-
Kwa waombaji wa shahada na stashahada: Umri kati ya miaka 18 na 30.
2. Elimu na Ufaulu
-
Kidato cha Nne: Awe na daraja la I hadi IV, na kwa daraja la IV, alama ziwe kati ya 26 hadi 28.
-
Kidato cha Sita: Awe na daraja la I hadi III.
-
Astashahada, Stashahada, na Shahada: Awe amehitimu katika fani zinazohitajika na Jeshi la Polisi.
3. Afya na Maumbile
-
Awe na afya njema ya kimwili na kiakili, iliyothibitishwa na daktari wa serikali.
-
Wanaume: Urefu usiopungua futi 5 na inchi 8 (5’8″).
-
Wanawake: Urefu usiopungua futi 5 na inchi 4 (5’4″).
4. Tabia na Maadili
-
Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
-
Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
-
Awe hajaoa/kuolewa na hana mtoto.
-
Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya polisi.
-
Awe tayari kufanya kazi za polisi popote nchini Tanzania.
-
Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili.
Mchakato wa Kutuma Maombi
1. Andika Barua ya Maombi
-
Waombaji wanatakiwa kuandika barua ya maombi kwa mkono wao wenyewe (handwriting).
-
Barua hiyo itumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkuu wa Jeshi la Polisi
S.L.P 961
DODOMA
2. Tuma Maombi Kupitia Mfumo wa Mtandao
-
Tembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi: https://ajira.tpf.go.tz
-
Jaza fomu ya maombi kwa umakini.
-
Pakua na ambatisha nyaraka zifuatazo:
-
Barua ya maombi.
-
Vyeti halisi vya elimu.
-
Cheti halisi cha kuzaliwa.
-
Kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa Taifa.
-
Picha ndogo (passport size) 6 zenye mandharinyuma ya buluu.
-
Nakala 5 za kila cheti kilichoainishwa.
-
3. Tarehe Muhimu
-
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 4 Aprili 2025.
Vifaa Muhimu kwa Mafunzo ya Polisi
Kwa waliochaguliwa, wanatakiwa kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 12 Juni 2025 hadi 14 Juni 2025. Vifaa muhimu vya kuleta ni pamoja na:
-
Mavazi ya mazoezi na malazi.
-
Traki suti ya rangi ya buluu yenye ufito mweupe.
-
Fulana nyeupe isiyo na maandishi.
-
Raba na soksi buluu.
-
Bukta mbili za buluu.
-
Sanduku la chuma (tranka) la rangi ya buluu.
-
Chandarua cheupe cha duara.
-
Shuka za rangi ya buluu mpauko jozi mbili.
-
Blanketi moja la kijivu lisilo na maua.
-
Pasi ya mkaa.
-
Vifaa vya usafi binafsi.
-
Vyeti halisi vya taaluma.
-
Cheti halisi cha kuzaliwa.
-
Kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa Taifa.
-
Nakala za kadi au namba za NIDA za wazazi na ndugu wa karibu.
-
Picha ndogo (passport size) 6 zenye mandharinyuma ya buluu.
-
Nakala 5 za kila cheti kilichoainishwa.
-
Kadi ya Bima ya Afya (NHIF) kama anayo au fedha taslimu.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
1. Je, ni lini mwisho wa kutuma maombi?
-
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 4 Aprili 2025.
2. Je, naweza kuomba kwa njia ya posta au barua pepe?
-
Hapana. Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe (email) au kwa mkono hayatapokelewa.
3. Je, ni fani gani zinazohitajika kwa waombaji wa shahada na stashahada?
-
Fani zinazohitajika ni pamoja na: Sheria, Usalama wa Mtandao na Uchunguzi, Sayansi za Afya (Madaktari, Uuguzi, Uuguzi wa Wanyama, n.k.), Uhandisi (Ujenzi, Umeme, Mitambo, Programu, n.k.), Sayansi ya Kompyuta na Teknolojia ya Habari, Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Dawa za Wanyama na Sayansi ya Wanyama, Uhandisi wa Baharini na Sayansi ya Bahari.
4. Je, ni lini nitajua kama nimeshinda usaili?
-
Majina ya waliochaguliwa hutangazwa kupitia tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi na vyombo vya habari.
5. Je, ni vifaa gani vya kuleta kwa mafunzo?
-
Vifaa vinavyohitajika ni pamoja na mavazi ya mazoezi, traki suti, fulana nyeupe, raba, soksi, bukta, sanduku la chuma, chandaruwa, shuka, blanket, pasi ya mkaa, na vifaa vya usafi binafsi.